Header Ads Widget

SERIKALI YAOMBWA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KUOKOA MAISHA YA WANAWAKE NA WATOTO AMBAO WAMEKUWA WAKIATHIRIKA NA MIGOGORO HIYO


Rose Njilo Mkurugenzi wa shirika la kutetea wanawake na watoto la MIMUTIE akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

Mwandishi wetu, ARUSHA

SERIKALI ameombwa kutatua migogoro ya ardhi Ngorongoro, ili kuokoa maisha ya maelfu ya wanawake na watoto ambao wamekuwa wakiathirika na migogoro inayoendelea.

Mkurugenzi wa shirika la utetezi wa wanawake na watoto la MIMUTIE, Rose Njilo akizungumza na waandishi wa habari baada leo ya kikao cha mashirika ya utetezi wa wanawake na watoto Ngorongoro, alisema Wanawake na watoto wamekuwa wakipata shida ya migogoro inayoendelea.

Alisema wanawake wanakosa utulivu na amani,watoto hawaendi shule, hakuna huduma bora za afya na maji hizi ni changamoto ambazo zinatokana na migogoro ardhi isiyokwisha Ngororongoro.

Njilo alisema mashirika ya utetezi wa haki za wanawake na watoto, wana imani kubwa na Rais Samia Suluhu kuwa anaweza kurejesha furaha na amani kwa wanawake na watoto wa Ngorongoro na kuuingilia kati migogoro ya ardhi.

"sisi tunaomba huduma muhimu zitolewe Ngorongoro, amani na utulivu virejeshwe kwa kila mara migogoro imekuwa ikibuliwa na wanaopata shida ni wananawake na watoto"alisema Njilo.

Mariam Kibore, Mkazi wa Ngorongoro, alitaka serikali kutatua shida za wanawake wa watoto wa Ngorongoro kwani wanaoshi maisha magumu, ikiwepo kukosa huduma muhmu.

"tunaomba serikali itusaidie sisi wanawake, kuondokane na hofu kila siku hatujuwi kesho itakuwaje, watoto hawasomi shule kwa amani"aliongeza.

Turane Mollel alitaka haki za wanawake na watoto kuzingatia Ngorongoro kwani wao ndio wapo majumbani muda mrefu na hawana na hawapati huduma muhimu.

Post a Comment

0 Comments