Header Ads Widget

MTUHUMIWA UJANGILI ALIVYODAKWA NA MKIA WA TWIGA


 
Mtuhumiwa wa ujangili idd Ally Iddy akiwa amekamatwa na mkia wa Twiga

Na Mwananchi wetu, BABATI

MTUHUMIWA wa ujangili Idd Ally Idd mkazi wa kijiji cha Mamire , wilaya ya Babati, mkoa Manyara amekamatwa akiwa na mkia wa Twiga baada ya kudaiwa kuwinda twiga na kuuza nyama kwa wananchi.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa katika operesheni za kupambana na majangili, katika eneo la ikolojia ya hifadhi ya Taifa ya Manyara- Tarangire na inayofanywa na kikosi maalum ambacho kinachoundwa na askari wa Mamlaka ya usimamizi wanyamapori(TAWA) askari wa burunge WMA , na askari wa Chemchem association ambao wameweza eneo la burunge WMA.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa wa kikosi cha kupambana na ujangili wa TAWA ambaye anaratibu Operation eneo hilo Pius William amesema tayari mtuhumiwa huyo amekabidhiwa polisi

"nikweli tumemkamata huyo mtuhumiwa na tayari mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea kufanyika "amesema William.

Akizungumzia kukamatwa mtuhumiwa huyo meneja wa Taasisi ya chem chem, Walter Pallangyo amesema kukamatwa mtuhumiwa huyu ni mkakati kudhibiti ujangili unaoendelea.

"Askari walikuwa wanafatilia kwa muda taarifa za mtuhumiwa huyo ndipo waliandaa mtego uliofanikiwa kumkamata akiwa na mkia "ameongeza.

Kikosi maalum kupambana na ujangili katika wilaya ya Babati kwa miezi minne sasa kimekamata watuhumiwa watano wa ujangili,wakiwepo waliokutwa na meno na tembo na nyara za serikali ikiwepo ngozi za pundamilia.

Watuhumiwa hawa wakikamatwa Katika operation ambazo zinaendelea kutokea kwenye eneo la hifadhi ya wanyamapori ya jamii ya Burunge, ambayo ipo katikati ya hifadhi za Tarangire na Manyara.

Post a Comment

0 Comments