Header Ads Widget

 KAMPUNI YA JAMBO FOOD PRODUCT YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA
TIMU YA  STAND UNITED 


Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo
Food Products, ambaye ni Meneja wakiwanda hicho upande wa uzalishaji
Hamduni Nasoro akimkabidhi katibu wa stend united ,Omary Malula
 
 NA AMOS JOHN

Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Ltd imetoa msaada wa
vifaa vya michezo ikiwemo jezi za kisasa vye thamani ya shilingi
milioni 2 kwa uongozi wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Stand united chama
lawana ukiwa nimkakati wakuiungamkono timu hiyo ili iweze kufanya
vizuri katika mashindano ya mbingwa wa mikoa ili hatimaye timu hiyo
iweze kurudi ligi daraja la pili hatimaye ligi kuu.

Timu ya Stand united Chama lawana nimiongoni mwatimu za mpira wamiguu
zilizo wahi kushiriki mashindano ya ligi kuu Tanzaniabara na hatimaye
kushuka daraja hadi kufikia ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa ambapo
kwa sasa timu hiyo inashiriki mashindano ya mambingwa wamikoa ili
baada ya kufuzu iweze kurudi ligi daraja la pili .

 Hafla fupi ya Makabidhiano ya vifaa vya michezo imefanyika February
18, 2022 katika ofisi kuu za kiwanda cha Jambo zilizopo Ibadakuli
mjini Shinyanga.

 Akikabidhi vifaa hivyo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo
Food Products, ambaye ni Meneja wakiwanda hicho upande wa uzalishaji
Hamduni Nasoro alisema Kampuni ya Jambo imeona ni vyema kusaidia vifaa
vya michezo ili kuongeza nguvu na kuwapa hamasa wachezaji wafanye
vizuri katika michuano ya Ligi ya mabingwa yanayo tarajia kuanza
kutimua vumbi katika dimba la Uwanja wa Taifa wilayani Kahama mkoani
humo.

 "Msaada huu hautoshi, tunapenda kuona wadau wengine wakijitokeza
kuisaidia timu hii ambayo imeonyesha nia ya kung’arisha nyota ya mkoa
wa Shinyanga katika medani za mpira wa soka," alisema Hamduni.

Kwa upande wake,katibu watimu hiyo kwa sasa Omary Malula aliishukuru
Kampuni ya Jambo Food Products Ltd kwa kuishika mkono timu hiyo na
kueleza kuwa timu iko vizuri na imara kushiriki vyema Ligi ya mabingwa
wamikoa na kuupaisha mkoa wa Shinyanga katika medani za soka kwa
ushindi na kupanda daraja kwenda daraja la pili huku akiomba wadau
wasoka wajitokeze kuiungamkono timu hiyo.

Naye, Kocha Mkuu wa Stand united Ally Mgazija ametamba kuwa timu yake
iko imara na hakuna timu itakayoizuia kuubeba ushindi wa ligi hiyo,
huku wachezaji nao wakitamba kuchukua ubingwa wa ligi hiyo
inayotarajiwa kuanza February 25 mwaka huu.

 Katika makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa Timu ya Stand united ,
pia Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, baada ya kukabidhi vifaa vya
michezo kwa Timu hiyo imeahidi kuendelea kuisaport timu hiyo ili iweze
kufanya vizuri katika mashindano hayo.

 

 

 

 

 


 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807