Header Ads Widget

SHIRIKA LA WEADO LATOA MAFUNZO YA KUIMARISHA UJENZI NGUVU ZA PAMOJA WA TAPO LA SHINYANGA

SHIRIKA LA WEADO LATOA MAFUNZO YA KUIMARISHA UJENZI WA NGUVU ZA PAMOJA WA TAPO LA SHINYANGA

Judith Kalwani -Mjumbe wa bodi wa shirika la WEADO akifungua kikao cha mafunzo ya kuimarisha ujenzi wa nguvu za pamoja la Tapo la Shinyanga.

 Maimuna Kanyamala,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la mikono yetu ambaye pia ni mkufunzi wa mafunzo ya ufeminist na nguvu ya Tapo akizungumza wakati wa mafunzo.

 Na mwandishi wetu.

Asasi za kiraia zipatazo 28 zinazojihusisha na shughuli za kutokomeza ukatili ndani ya mkoa wa Shinyanga zimepatiwa mafunzo ya ufeminist na kuimarisha ujenzi wa nguvu za pamoja la TAPO la Shinyanga na shirika la WEADO kwa ajili ya kuongeza uelewa wa kupambana na ukatili wa kijinsia mkoa wa Shinyanga.

Asasi hizo za kiraia zimepatiwa mafunzo leo, jumamosi tarehe 19 Februari ,2022 katika ukumbi wa hotel ya katemi iliyopo manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuimarisha ujenzi wa nguvu ya pamoja ya TAPO (Umoja wa asasi za kiraia wa kutetea haki za wanawake) kwa mkoa wa Shinyanga.

Akifungua mafunzo hayo, Judith Kalwana kwa niaba ya Mkurugenzi wa shirika hilo, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya WEADO, amesema ni muhimu kukutana pamoja kwani ukatili wa kijinsia bado unaendelea na ni wajibu wetu kutokomeza ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga.

“Hali ya ukatili wa kijinsia ndani ya mkoa wa shinyanga si suala la kuuliza kwani mila na desturi bado zinachochea ila ni jukumu letu si kama asasi za kiraia kuona usalama na amani kwa wanawake na watoto.

Mkoa wa Shinyanga ni miongoni wa mkoa kinara yenye changamoto ya ukatili dhidi wanawake na watoto. Kwa mujibu wa Takwimu za shirika la watoto (UNICEF 2012) mkoa wa Shinyanga una asilimia 59 kwa ndoa za utotoni, ikifuatiwa na Tabora 58, Mara 55, Dodoma 51, Lindi 48, Mbeya 45, Morogoro 42, singida 42, Rukwa 40, Ruvuma 39, Mwanza 37, Kagera 36, Mtwara 53 na Manyara 34.

 Maimuna Kanyamala, Mkurugenzi wa wa asasi ya Mikono Yetu ambaye pia ni mkufunzi wa mafunzo hayo alisema kuwa changamoto kubwa ya sasa kukosekana kwa historia ya nyuma inayo elezea juhudi za wanawake katika jamii juu ya mafaniko mbalimbali.

“Vijana wa sasa hawatambui nafasi ya mwanamke kutokana na historia za nyuma kutomwandika mwanamke kwa upana zaidi, Kalamu ingemwandika mwanamke leo hii vizazi vingejifunza kuona nafasi ya mwanamke katika mabadiliko ndani ya jamii” Alisema Maimuna.

Aidha, Maimuna aliongeza kwa kusema ni “wakati wa TAPO kuwa na ubunifu wa mbinu na mikakati ya kiutendaji ili kuweza kuleta mabadiliko na si vema kuwa wa kizamani tena

Leah Josiah wa Shirika la Fikra Mpya alisema kuwa hali ya kujitambulisha ndani ya jamii kuwa ni mfeminist inaleta ugumu kwa mapokeo ya jamii na kuonekana kama ni mtu mkorofi, Hii inatokana na jamii kutokuwa na uelewa wa kutosha.

Kwa upande wake, Kareny Masasy mwandishi wa habari aliyeshiriki mafunzo hayo alisema kuwa jamii ina uelewa hafifu hasa tunapotumia kalamu zetu kuandika changamoto za wanawake maeneo ya vijijini kwani tunaonekana ni maadui hasa kwa wanasiasa kwa kuibua yale mabaya yanayo wahusu wanawake.

 

Salome Shangari,Afisa mradi kutoka shirika la WEADO akitoa ufafanuzi wa zaidi juu ya mafunzo hayo kuhusu dhana ya TAPO  na umuhimu wa mada hiyo.

 

 Veronica Massawe,Mkufunzi kutoka shirila la Young Women Leadership akitoa mada ya kuhusu ulagibishaji katika kuhusiana na jamii.

 Paschalia Mbugani,Mkufunzi kutoka  shirika la Thubutu Africa Initiative akitoa mada katika mafunzo.

  Rashida .S.Massawe mfuatiliaji na tathimini kutoka asasi ya WEADO akichukua kumbukumbu za shughuli za mafunzo.

  Pendo Sawa katibu kutoka asasi ya wanawake 100,000 akiwasilisha mada ya maana ya jinsi katika mafunzo.

Deborah Lameck ,Mkurugenzi wa Teengers Foundation Tanzania akiwasilisha majibu ya mada ya ufeminist.

 Mussa Ngangara,Mkurugenzi wa shirika la TVMC akiwasilisha mada inayohusu utetezi wa kifeministi.
Annastazia Donald kutoka shirika la Right to life akiwasilisha majibu ya maswali kuhusu maana ya Tapo.
 
Leah Josiah,Mkurugenzi wa asasi ya Fikra Mpya akiwakilisha kuhusu mada ya mikakati ya Tapo.
 
 Khalfan Ali mwakilishi wa shirika la Redcross mkoa wa Shinyanga akiwasilisha kuhusu mikakati ya Tapo la Shinyanga.

Mariam Saguda mwakilishi wa asasi ya kirai ya OPE mkoani Shinyanga akiwasilisha mada kuhusu mikakati ya Tapo.

John Eddy kutoka shirika la Young Women Christian Assocition akitoa uwasilishaji wa kundi lake wakati wa mafunzo ya WEADO.

Mariam Maduhu mwakilishi wa asasi ya RAFIKI SDO akiwasilisha mada juu ya mikakati ya Tapo.

Paulo Amos kutoka asasi ya  life with hope foundation akiwasilisha mada kuhusu shughuli ya utetezi.

Nkinda Shada Joseph mwakilishi wa shirika la Women Beyond Limits akiwasilisha mada ya kuhusu mikakati ya Tapo.


 SHUGHULI ZA VIKUNDI KATIKA MAFUNZO.



Post a Comment

0 Comments