Header Ads Widget

MAKAMANDA WA JESHI LA POLISI WAPANGULIWA

sirropicMkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo ya makamanda wa Jeshi la Polisi wa mikoa kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo.


Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Februari 3, 2022 na msemaji wa jeshi hilo, David Misime imeeleza kuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Wankyo Nyigesa amehamishwa kutoka mkoa wa Pwani kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera.

“Kamanda Nyigesa amechukua nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa mkoa huo, Awadhi Juma Haji ambaye Januari 31, 2022 alipandishwa cheo kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa Kamishna wa Polisi (CP) na pia kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan” imeeleza taarifa hiyo.

 SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANACHI

 

TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807