` JAMBO AMUOMBEA KURA,RAIS SAMIA,KATAMBI NA SALUM KITUMBO

JAMBO AMUOMBEA KURA,RAIS SAMIA,KATAMBI NA SALUM KITUMBO

 


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Meatu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Salum Khamis maarufu Jambo,amemuombea kura nyingi za ushindi Mgombea Urais wa CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi na Mgombea Udiwani Kata ya Mjini Salum Kitumbo.

Ameomba kura hizo leo Oktoba 17,2025, kwenye Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Udiwani wa Kata ya Shinyanga Mjini Salum Kitumbo,uliofanyika viwanja vya Soko Kuu la Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na Mamia ya wananchi.
Amewaomba wananchi kwamba,siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 wajitokeze kwa wingi kupiga kura na wasifanye makossa,bali wakampigie kura nyingi za Ushindi Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,Patrobas Katambi,pamoja na Salum Kitumbo,ili wapate kuwaletea maendeleo sababu ni viongozi makini na wenye kujali maslahi ya watu.

“Ndungu zangu wananchi wa Shinyanga Mjini,Oktoba 29 nendeni mkapige kura sababu ni haki yenu ya msingi na mkawachague wagombea wote wa CCM kuanzia Ngazi ya Rais,Wabunge na Madiwani,”amesema Khamis.
Aidha,akimzungumzia Rais Samia,amesema ndani ya utawala wake wa miaka mitano iliyopita amefanya mambo makubwa hapa nchini, pamoja na kuiletea maendeleo Kata ya Shinyanga Mjini,huku akimpongeza pia Patrobas Katambi, kwamba ni kiongozi mzuri ambaye ameaminiwa na Rais, na ameubadilisha mji wa Shinyanga na wanastahili kupewa mitano tena.

Amesema kwa upande wa Sulum Kitumbo,amesema anamfahamu vizuri na kwamba Kata ya Shinyanga Mjini imepata Diwani ambaye ni mchapakazi,Mwaminifu,Mwadilifu na ambaye anajali maslahi ya watu sababu amefanya naye kazi siku nyingi na anamfahamu vizuri.
“Salum Kitumbo na simama hapa kukuombea kura kwa wananchi wa Shinyanga Mjini,naimani watakupatia ridhaa ya kuwa diwani wao,na kazi ya udiwani ni utumishi wa watu nakuomba sana uwatumike wananchi,simu zipatikane na nyumbani kwako upatikane shughulikia matatizo ya wananchi na uwaletee maendeleo nafahamu utendaji wako kazi,”amesema Khamis.

Naye Mgombea Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini Salum Kitumbo,akimwaga sera kwa wananchi wameahidi kwamba atakamilisha ujenzi wa Soko Kuu la Mjini humo ili kuboresha mazingira rafiki kwa wafanyabiashara.

Ametoa ahadi nyingine kwamba barabara zote za mjini humo zitajengwa kwa kiwango cha lami katika mitaa yote, huku akiwahidi pia kusimamia vyema suala la mikopo ya halmashauri asilimia 10 ili makundi husika ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wapate kunufaika nayo na kuinuka kiuchumi.

TAZAMA PICHA👇👇
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis akizungumza kwenye Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini Salum Kitumbo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis (kulia)akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Shinyanga Mjini Salum Kitumbo.
Mgombea Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini Salum Kitumbo akinadi sera kwa wananchi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis,akisalimiana na wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni.













Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464