` WALIMU WANAWAKE MANISPAA YA SHINYANGA WASHIRKIKI KONGAMANO LA KUWAJENGEA UWEZO WA KUKABILIANA NA VITENDO VYA UKATILI WAKIJINSIA KWA WANAFUNZI MASHULENI

WALIMU WANAWAKE MANISPAA YA SHINYANGA WASHIRKIKI KONGAMANO LA KUWAJENGEA UWEZO WA KUKABILIANA NA VITENDO VYA UKATILI WAKIJINSIA KWA WANAFUNZI MASHULENI

 

Na Mwandishi wetu kutoka Mkoani Shinyanga.

Walimu wanawake wa Manispaa ya Shinyanga wamehimizwa kutumia utu na weledi wao kupinga na kuzuia ukatili wakijinsia kwa wanafunzi mashuleni huku wakishauriwa kuwa karibu na watoto hao ili kuzuia ukatili wakijinsia ambao unatajwa kuanza kuongezeka siku hadi siku mashuleni na mitaani.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya wanawakeke Laki Moja Mkoani Shinyanga Bi. Anascolastica Ndagiwe leo tarehe 24 Oktoba. 2025 wakati akiwasilisha mada ya ukatili wakijinsia kwenye kongamano la kuwajengea uwezo walimu wanawake wa manispaa ya Shinyanga,  kongamano ambalo limehusisha mada mbalimbali ikiwemo Ukatili wakijinsia, Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, Mirathi na Talaka, uchumi na Mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na taasisi za fedha ikiwemo NMB.

Bi. Anascolastica Ndagiwe, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja Mkoa wa Shinyanga akitoa mada ya Ukatili wakijinsia.

Afisa Utumishi Manispaa ya Shinyanga Bw. Jackson Mwakisu amesema walimu wanawake wana wajibu wa kulilea Taifa kwakuwa wana nafasi pana kama walezi kwenye upande wa uchumi wa familia zao na kuutaka uongozi wa kitengo cha walimu wanawake kuendeleza makongamano yakuwajengea uwezo kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa maendekeo.

Bw. Jackson Mwakisu, Afisa Utumishi Manispaa ya Shinyanga akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexus kagunze aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye Kongamano hilo 

Nao baadhi ya walimu waliojenmgewa uwezo akiwemo Mwl. Leah Makaranga mwakilishi wa Elimu wanawake Mkoa wa shinyanga na Namsifu Mndeme wa Shinyanga Manispaa wamesema kongamani hilo limewafunza mambo mengi na wamepata faida kwakuwa wamejifunza mambo mengi ambayo yatawasaidia katika kulinda maadhili ya familia zao.

kwa upande wa Mada ya sheria ya Ndoa na mirathi, mwanasheria Ruth Ndagu amesema kuna umuhiku kwa walimu wanawake kuijua sheria hiyo vyema ili kukabikliana na mazingira ya kukosa mirathi endapo ikitokea bahati mbaya kupoteza mweza lakini pia kufahamu haki zao za kisheria katika maisha yao na watoto wao.

Ruth Ndagu (Mwanasheria) akitoa mada ya Sheria ya ndoa ya Mwaka 1971 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwenye kongamano hilo la walimu wanawake.

Mwenyekiti wa chama cha walimu kitengo cha walimu wanawake Manispaa ya Shinyanga Mwl. Subira Mustafa Kuhenga asema kupitia kongamano hilo ambalo limeandaliwa na kitengo cha walimu wanawake manispaa ya Shinyanga wanawake na walimu kwa ujumla wana nafasi kubwa ya kupinga na kuzuia ukatili kwa wanafunzi wakike na wakiume huku akiwataka wadau na taasisi mbalimbali zinazojuhusisha na utetezi wa haki za Binadamu kutembelea mashuleni kutoa elimu kwa wanafunzi na walimu juu ya kuepuka ukatili na hatimaye kupunguza ukatili kama sio kuutokomeza kabisa.

Elizabeth Werema ni Katibu wa Kitengo cha Walimu wanawake Taifa amewahamasisha walimu wanawake kuhakikisha kila mmoja anaanzia nyumbani kwake kuzuia na kupinga ukatili wakijinsia na kukazia kuwa Mwalimu mwanamke kama mama na kama mlezi kufanya urafiki wa karibu na watoto ili kuweza kuangalia hali zao za kila siku kuona endepo kuna unyanyasaji wa kijinsia kwakuwa unyanyasaji wa kijinsia pia hufanyika majumbani kwa ndugu na jamaa kwa hiyo kupitia ukaribu huo wanaweza kugundua kama kuna unyanya saji umefanyika.

Naye Mwal. Monica Makulo mgeni mualikwa kutoka Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza amesema amefurahi sana kushiriki kongamano hilo ambalo limefundisha mbinu mbalimbali za kuwasimamia watoto katika harakati za kupinga ukatili wakijinsia kubwa zaidi ni uwajibikaji wa maadili katika upande kazi zao.

Mjumbe wa kamati tendaji wa chama cha walimu Taifa Bi. Grace Kulwa amesema kongamano hilo limefungua njia kwa upande wa walimu wanawake kujenga mahusiano mazuri kazini, ujasiriamali na uwekezaji hali ambayo inaende kubadilisha maisha ya familia za walimu wa manispaa ya shinyanga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitengo cha Walimu Wanawake Taifa Bi. Neema Obedi amesema walimu watakapokuwa na uelewa mzuri na mpana wataweza kulea kizazi bora cha Watanzania ambao ni vuongozi wa keshi kwahiyo kongamano hilo limekuwa na faida kubwa sio kwa walimu wanawake tu bali kwa walimu wote na wanafunzi wanaowafunzisha mashuleni.

Samwel Jackson, Mwakilishi wa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na wenye ulemavu Mh. Patrobas katamni akizungumza na walimu Wanawake kwenye kongamano hilo






































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464