Header Ads Widget

MADIWANI SHINYANGA WAPITISHA MAPENDEKEZO YA BAJETI SHILINGI BILIONI 34.8/-


Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao Maalum cha baraza cha kupitia mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri ya mwaka wa fedha (2022-2023) Sh.bilioni 34.8

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wamepitisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha ya Halmashauri (2022-2023) kiasi cha Sh.bilioni 34.8.

Madiwani wamepitisha mapendekezo ya mpango na bajeti leo januari 27, 2022, kwenye kikao maalum cha kujadili na kupitia mapendekezo ya mpango huo wa bajeti ya mwaka wa fedha (2022-2023).

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza mara baada ya madiwani kumaliza kupitisha mapendekezo ya mpango huo wa bajeti, amewaasa wataalam pamoja na madiwani, kushirikiana pamoja kuibua vyanzo vipya vya mapato, ili kufikia lengo la Manispaa hiyo kukusanya fedha za mapato ya ndani Sh.bilioni 4.6.

Alisema katika Manispaa hiyo kuna vyanzo vingi vya mapato ambavyo havitambuliki na havikusanywi mapato yake, na kuomba vifuatiliwe ili Serikali ipate mapato ambayo yatatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

“Bajeti yetu madiwani mmeiona ambapo katika mapato yetu ya ndani tunapaswa kukusanya kiasi cha fedha Sh.bilioni 4.6, hivyo tujitahidi kwenye ukusanyaji wa mapato pamoja na kuibua vyanzo vipya,”alisema Masumbuko.

Aidha, alitoa wito kwa madiwani wa Manispaa hiyo, waendelee kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao, ili miradi hiyo itekelezwe kwa kiwango kinachotakiwa na thamani ya fedha ionekane.

Nao baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakichangia bajeti hiyo, walibainisha baadhi ya vyanzo vipya vya mapato, ambavyo vinapaswa kufuatiliwa na kuanza kukusanywa mapato, ikiwamo minada ya kuuza mbuzi ambayo haikusanywi mapato yake.

Awali Kaimu Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Fidelis Kabuje, akisoma mapendekezo ya mpango huo wa Bajeti ya mwaka wa fedha (2022-23) alisema mapendekezo ya bajet katika Manispaa hiyo ni Sh.bilioni 34.8.

Alifafanua kuwa vyanzo vya mapato ya ndani ni Sh.bilioni 4.6, Ruzuku ya matumizi mengine bilioni 1.04, Ruzuku Mishahara bilioni 19.4, Ruzuku miradi ya maendeleo kutoka Serikali kuu bilioni 3.5, Ruzuku miradi ya maendeleo kutoka kwa wahisani Sh.bilioni 6.1.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye baraza hilo maalumu la kujadili kupitia mapendekezo ya mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha (2022-2023).

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akizungumza kwenye Baraza hilo.

Kaimu Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Fidelis Kabuje, akisoma mapendekezo ya mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha (2022-2023) kwenye Baraza la madiwani Manispaa ya Shinyanga.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao maalumu cha Baraza la kupitia mapendekezo mpango na Bajeti wa mwaka wa fedha (2022-2023).

Madiwani wakiendelea na kikao maalum cha Baraza.
Madiwani wakiendelea na kikao maalum cha Baraza.

Madiwani wakiendelea na kikao maalum cha Baraza.

Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.

Madiwani wakiendelea na kikao cha Baraza.

Madiwani wakiendelea na kikao maalum cha Baraza.

Madiwani wakiendelea na kikao maalum cha Baraza.

Wataalam wakiwa kwenye Baraza hilo maalum la Madiwani.

Wataalam wakiwa kwenye Baraza hilo maalum la Madiwani.
Wataalam wakiwa kwenye Baraza hilo maalum la Madiwani.

Wataalam wakiwa kwenye Baraza hilo maalum la Madiwani.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments