Header Ads Widget

TRA WAZIBURUZA MAHAKAMANI KAMPUNI MBILI, MADAI KUSHINDWA KUTOA RISITI KWA WATEJA


Picha Mashine ya Risiti ya kielekitronic

Suzy Luhende, SHINYANGA

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani Shinyanga imezifikisha Mahakamani kampuni mbili za wafanyabiashara kutokana na madai ya kushindwa kutoa risti za kieletroniki na kusafirisha bidhaa bila kuweka stempu pamoja na mteja mmoja kwa kosa la kutodai risti ya bidhaa alizonunua zenye thamani ya Sh18,000.

Akisoma mashitaka ya wafanyabiashara hao Hakimu Mkadhi Mfawidhi Mkoa wa Shinyanga Merry Mrio ,amesema Meneja mauzo kutoka Kampuni ya Jambo food Product Pendo Saguda amesema alishitakiwa kwa kosa la kutoa risti ya Sh 18,000 kwa mteja wake Boniface Magadula,aliyemuuzia bidhaa ambapo baada ya kusomewa shitaka lake amekiri kosa na kupewa adhabu ya kulipa Sh 3 milioni au kifungo cha miezi sita jela.

Kampuni hizo ambazo zimefikishwa mahakamani ni Jambo food Product,na Tunel Corparation Limited za Mkoani Shinyanga zimefikishwa katika mahakama hiyo ya hakimu mkazi Mkoa wa Shinyanga na kusomewa makosa yao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Tunel Corparation Limited Tumusime Tibaijuka amekana shitaka hilo na kesi yake namba 56 ya mwaka 2021 imepangwa kusikilizwa tena Desemba 15 mwaka huu,huku mahakama ikiagiza kutafutwa Boniface Magadula kutokana na kushindwa kufika Mahakamani hapo.

Mwanasheria mwandamizi wa serikali Maricel Busegano amesema watuhumiwa hawa kabla ya kupelekwa mahakamani waliandikiwa barua kuwa wafike ofisi za TRA ndani ya siku Saba lakini hawakufanya hivyo, na baada ya siku hizo kuisha walipelekwa mahakamani.

Post a Comment

0 Comments