Header Ads Widget

TFF/ CAF/ FIFA/ SABABU KOCHA WA SIMBA QUEENS KWENDA KUSOMA


Kocha Msaidizi wa timu ya Simba Queens MattyDiola amesema moja Kati ya ndoto zake ni kuwa na Elimu ya ukocha ya kutosha kulingana na vigezo vya TFF/CAF/FIFA wanavyovitaka.

Akizungumzia kuhusiana na taarifa zilizosikika kuwa anaenda kusoma, Kocha MattyDiola amesema ni kweli anaenda kusoma course ya Leseni B ya CAF ambayo amekuwa anaitamani kuipata muda mrefu.
MattyDiola ameweka wazi kuwa anaondoka leo kuelekea mjini Morogoro sehemu ambayo kozi ya Leseni B (CAF) itatolewa na tayari maandalizi na malipo ya kozi ameshayakamilisha.

"Namshukuru Mungu kwa hatua hii, nilikuwa na ndoto za kuendelea kuongeza Elimu ila muda ulikuwa bado haujafika, nafurahi muda umefika niende kusoma" alisema Kocha MattyDiola.

"Ninawashukuru Viongozi wangu wa 𝘀𝗶𝗺𝗯𝗮 sports club kunipa ruhusa ya kwenda kusoma, nawashukuru wasimamizi wangu kuhakikisha napata nafasi hii adhimu Katika maisha yangu ya Soka" Alisema MattyDiola.

Kocha MattyDiola ni Kocha aliye na nia ya kufika mbali kitaaluma. Amekuwa na hamu ya kutaka kusoma zaidi ya hatua aliyonayo Ili kumuongezea wigo wa kujiamini zaidi kwa Kila anachokifanya.

Kocha Matty Diola alijiunga na Simba Queen Msimu uliopita akitokea Jakaya Mrisho Kikwete (JMK Academy) akiwa Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake.

Baada ya Kujiunga Simba Queens, Kocha MattyDiola alikuwa Msaidizi wa Kocha Mussa Hassan "Mgosi" na kwa ushirikiano walitwaa Kombe la ubingwa Ligi ya Wanawake Tanzania.

Baada ya kutwa ubingwa, Simba queens ikiwa chini ya kocha mpya Hababuu akishirikiana na MattyDiola kwenye mashindano ya women’s champions league yaliyofanyika nchini Kenya(Nairobi.)

Pamoja na kutopata matokeo mazuri, Kocha Matty Diola aliendelea kutoa ushirikiano Kwa Kocha Hababu mpaka pale Uongozi wa Simba Queens ulipomweka pembeni na nafasi yake kuchukuliwa na Kocha Sebastian Mkoma.

MattyDiola ni moja ya Makocha wa Kike Nchini Tanzania wenye heshima kubwa kutokana na jitihada anazozionyesha kwenda nafasi yake ya ukocha Msaidizi wa Timu ya Simba Queens.
Post a Comment

0 Comments