Header Ads Widget

RESTLESS DEVELOPMENT WAENDESHA MJADALA OLDSHINYANGA, MABINTI, WAZAZI WAFUNGUKA CHANZO MIMBA ZA UTOTONI

Afisa Vijana wa Mradi Tunaweza kutoka Shirika la Restless Development Vick Vigero, akizungumza kwenye mjadala wa haki za vijana wa kike katika kuwapatia elimu ya afya ya uzazi, usawa wa jinisa na Stadi za maisha katika Kata ya Olshinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

SHIRIKA la Restless ambalo linatekeleza mradi wa Tunaweza kwa Mabinti 100 wenye uzao mmoja, na vijana wa kike 90, katika kuwapatia elimu ya afya ya uzazi, ujasiriamali na kuwajenga kuwa viongozi, wameendesha mjadala na wanajamii wa Olshinyanga kuhusu malezi ya watoto wa kike.
 
Mjadala huo umefanyika leo kwenye viwanja vya Zahanati ya Olshinyanga, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wananachi, pamoja na vijana, ambapo mjadala ulihusu mahitaji na haki za vijana katika kuwapatia elimu ya afya ya uzazi, usawa wa kijinsia, na stadi za maisha.

Afisa vijana wa Mradi Tunaweza kutoka Shirika la Restless Development Vick Vigero, akielezea malengo ya mjadala huo, amesema ni kuwekana sawa kati ya wazazi, viongozi, na wasichana, ili kuona wapi kuna tatizo (gepu) katika kuhakikisha mtoto wa kike hapati ujauzito na kutimiza ndoto zake.

Alisema mjadala huo umehusisha mabinti, wazazi, pamoja na viongozi wa Serikali, ili kupata suluhisho la kupunguza mimba za utotoni mkoani Shinyanga.

“Shirika letu la Restless Development tumekuwa tukitekeleza mradi wa Tunaweza, na kuhusisha mabinti wenye uzao mmoja, pamoja na mabinti wengine , ambapo hua tunawapatia elimu ya afya ya uzazi, kuwajenga kiuchumi na kuwa viongozi, ili wajitegemee katika maisha yao na kuumpa thamani mtoto wa kike ndani ya jamii,” alisema Vigero.

“Mradi wetu hapa nchini Tanzania tunautekeleza katika Mikao mitatu ambayo ni Dodoma, Simiyu na Shinyanga, na katika Manispaa ya Shiyanga tupo Ndembezi, Ndala na Olshinyanga, na tunafanya mjadala huu ili sisi tutakapo maliza mradi wetu, jamii na viongozi waendelee kuutekeleza kwa kuona wapi kuna mapungufu na kuyatafutia ufumbuzi na kumkomboa mtoto wa kike,”aliongeza.

Nao wazazi wakizungumza kwenye mjadala huo, walisema chanzo cha mimba za utotoni mkoani Shinyanga, husabishwa na baadhi ya wazazi kwa kushindwa kutekeleza majukumu kwa watoto wao, na wengine kuwageuza kama vitega uchumi vya familia kwa kupata mali au mifugo, huku wazazi wengine wakisema chanzo ni Mabinti wenyewe kwa kutaka vitu vizuri.

Mmoja wa wazazi hao Reokadia Pius, alisema baadhi ya mimba za utotoni zinasababishwa na matatizo ya kifamilia, ambapo wazazi hushindwa kulea familia zao vizuri, na kuwachia watoto wakijitawala na wao kuwa bize na maisha, huku wakishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri, ambapo watoto huamua kujitafutia mwenyewe na kujikuta akinasa ujauzito.

Naye mzazi Elizabeth Shindai, alisema baadhi ya wazazi ndiyo wamekuwa chanzo cha mimba za utotoni, kwa kuendeza masuala ya Rushwa kutoka kwa watuhumiwa wa mimba hizo, na kugeuza watoto wao kama vitega uchumi ambapo hupokea pesa ama mifugo na kumaliza kesi kimya kimya na kisha mtuhumiwa kuachiwa huru.

Kwa upande wake mzazi Edna Samweli, alisema mabinti wa siku hizi wameporomoka kimaadili, ambapo wamekuwa na tamaa ya kutaka vitu vikubwa kuliko uwezo wao, na hivyo kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi ili wapate pesa ya kununua Chipsi kuku, pamoja na simu za kupangusa (Smartphone) ambayo hata mzazi wake hana.

Nao mabinti waliwanyooshea vidole wazazi, kuwa baadhi yao wamekuwa chanzo cha wao kupata ujauzito, ambapo wamekuwa bize na maisha, na kushindwa kuwapatia elimu ya afya ya uzazi, huku wengine wakishindwa kuwatimizia mahitaji yao.

Kwa upande wake Mtendaji wa kijiji cha Ihapa Oldshinyanga Simon Mpaname, amelipongeza Shirika hilo kwa kuendesha mjadala huo, ambapo amesema utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya mimba za utotoni, huku akiwasihi wazazi kila mmoja atekeleze majukumu yake kwa watoto, na watoto wa kike wajitambue huku akiwaasa wale ambao hawasomi wajiunge kwenye vikundi ili wapate mikopo ya Halmashauri ya vijana asilimia 4 na kujiajiri wenyewe.

Katika hatua nyingine alitoa wito kwa mabinti, kuwa wawe wanahudhulia kwenye mikutano ya hadhara ya vijijini na kutoa kero zao ili zipate kutatuliwa, huku akiwasihi pia wawe wanajitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, ambapo zitawasaidia kuwa wanawasilisha changamoto za vijana wenzao na kutatuliwa.

Afisa vijana wa mradi Tunaweza kutoka Shirika la Restless Development Vick Vigero, akizungumza kwenye mjadala wa haki za vijana wa kike katika kuwapatia elimu ya afya ya uzazi, usawa wa jinisa na Stadi za maisha katika Kata ya Olshinyanga.

Amani Makalani Muelimishaji Rika kutoka Restless Development, akizungumza kwenye mjadala huo.

Magdalena Pitawaka mjumbe wa  Bodi ya ubalozi ya uswizi, akizungumza kwenye mjadala huo.

John Eddy Mwakilishi wa Shirika la Restless Development mkoani Shinyanga akizungumza kwenye mjadala huo.

Mtendaji wa kijiji cha Ihapa Olshinyanga Simon Mpaname, akizungumza kwenye Mjadala huo.

Wananchi wa Olshinyanga wakiwa kwenye mjadala huo.

Mabinti wa Olshinyanga wakifuatilia mjadala huo.

Mzazi Edna Samweli akichangia mjadala huo.

Mzazi Reokadia Pius akichangia mjadala huo.

Mzazi Peter Hungwi akichangia kwenye mjadala huo.

Mzazi Frola Mihambo akichangia mjadala huo.

Wananchi na vijana wakiwa kwenye mjadala huo.

Wananchi wa Olshinyanga wakiwa kwenye mjadala huo.

Wananchi wa Olshinyanga wakiwa kwenye mjadala huo.

Wananchi wa Olshinyanga wakiwa kwenye mjadala huo.

Wananchi wa Olshinyanga wakiwa kwenye mjadala huo.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.Post a Comment

0 Comments