Header Ads Widget

MWENYEKITI WA KITONGOJI AMUUA MKEWE KWA WIVU WA MAPENZI, NAYE AJINYONGAMwenyekiti wa kitongoji cha Urua chini,kijiji cha Mfuruashe wilayani Rombo,Agustine Moshi(35) amemuua mkewe, Anastasia Agustine (31) kwa kumkata kata na kitu chenye ncha kali na kisha mwenyewe kujiua kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
 
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mshereheshaji maarufu wilayani humo (MC), anadaiwa kutenda mauaji hayo usiku wa kuamkia leo Novemba 8, 2021.

Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo leo Novemba 8, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema wawili hao walikuwa na mgogoro wa kimapenzi, ambapo wiki moja iliyopita mke wake huyo alimpeleka dawati la jinsia Rombo.


SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI

Post a Comment

0 Comments