Header Ads Widget

MWANAMKE ADAIWA KUMUUA MUMEWAKE NA KISHA KUMZIKA KWENYE SHIMO LA KUCHOMEA MKAAWananchi wa kijiji cha Kabage Mashariki wakibomoa nyumba ya Mwenyekiti wa Kitongoji , Pagi Makashi anayedaiwa kumfuata mtuhumiwa na kumuomba Sh3 milioni ili awapelekee ndugu wa marehemu na kulifanya jambo hilo kuwa siri. Picha na Mary Clemence.

 Matukio ya mauaji ndani ya familia yanayohusishwa na wivu wa mapenzi na migogoro ya mali yameonekana kushika kasi nchini. Hiyo inafuatia mwanamke mmoja Limi Shija (55) mkazi wa Kijiji cha Kabage wilayani Tanganyika, kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya mumewe Masunga Kashinje (68) kisha mwili wake kuuzika katika shimo la kuchomea mkaa pembezoni na makazi yao.

Akizungmzia tukio hilo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho Kulwa Mhoja alikiri kutokea kwa mauaji hayo jana, huku akidai kuwa Kashinje alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu mwezi Mei 2021.

Amesema taarifa za mauaji ya Kashinje alizipata Julai 11,2021 saa 1:00 asubuhi kupitia kwa Afisa mtendaji wa kijiji hicho baada ya kumpigia simu na kumtaka afike nyumbani kwake.

 SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI

 

Post a Comment

0 Comments