Header Ads Widget

WAZAZI, WALEZI WAMETAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUWALEA WATOTO WAO KATIKA MALEZI BORA NA SIYO KUWATELEKEZEA WALIMU


Meneja Miradi kutoka Shirika la RAFIKI SDO Ahsante Nselu akizungumza kwenye Mahafali ya Shule ya Sekondari Mazinge.

Na Josephine Charles, SHINYANGA

Wazazi na Walezi mkoani Shinyanga, wametakiwa kutambua kwamba ni jukumu lao kuhakikisha wanafunzi wanasimamiwa katika malezi bora, kuanzia ngazi ya kaya, kwa lengo la kuwasaidia waalimu suala la malezi, pindi wanapokuwa shule, ili kupata elimu bora, pamoja na kuchochea hali ya ufaulu wa mtihani.

Hayo yameelezwa na Meneja Miradi kutoka shirika la Rafiki Social Development Organization(RAFIKI-SDO), bwana Ahsante Nselu aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Shirika hilo kwenye mahafali ya 12 ya Shule ya Sekondari ya Mazinge, iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ambapo ameshiriki kama mgeni Rasmi.

Bwana Nselu amesema. pamoja na mafanikio waliyonayo shule ya Mazinge zile changamoto ambazo zinarudisha nyuma maendeleo ya ufaulu, basi wao RAFIKI-SDO wameahidi kuchangia gharama zote za mtihani wa kidato cha nne mwaka huu.

Pia, amesema katika kuendeleza vipaji vya wanafunzi kwa upande wa michezo, ameahidi kutoa mipira miwili ya mchezo wa miguu, mipira miwili ya Pete, pamoja na kuchangia mifuko 10 ya Saruji, kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya madarasa ambayo imechakaa.

Awali Mkuu wa Shule hiyo Mwl James Msimba, alisema zipo changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo, ambapo yapo jumla ya matundu sita kwa wanafunzi wote 778, ambapo matundu manne yanatumiwa na wasichana na matundu mawili yanatumiwa na wavulana. hali inayopelekea foleni wanafunzi wakienda kujisaidia wakati wa mapumziko.

Mkuu huyo wa shule ya sekondari Mazinge ameiomba serikali na wadau wengine, kutoa msaada wa vitu mbalimbali ili kupunguza changamoto zinazoikabili shule hiyo.


Meneja Miradi kutoka Shirika la RAFIKI SDO Ahsante Nselu akizungumza kwenye Mahafali ya Shule ya Sekondari Mazinge.

Mkuu wa shule ya Sekondari Mazinge James Msimba akisoma Taarifa ya Shule.

Wahitimu kidato cha Nne wakiwa kwenye Mahafali yao.

Wahitimu kidato cha Nne wakiwa kwenye Mahafali yao.

Wahitimu kidato cha Nne wakiwa kwenye Mahafali yao.

Wahitimu kidato cha Nne wakiwa kwenye Mahafali yao.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali.Post a Comment

0 Comments