Header Ads Widget

VICTOR MMANYWA ATANGAZWA MSHINDI UCHAGUZI KATA YA NDEMBEZI

 

Mhe. Victor Thobias Mmanywa (CCM) akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa kuwania nafasi ya udiwani kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga. Picha na Amos John

****
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Timothy Andrew Timothy amemtangaza na kumkabidhi cheti cha ushindi Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi Victor Thobias Mmanywa wa Chama Cha Mapinduzi kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa kuwania nafasi ya udiwani kata ya Ndembezi.

Akimkabidhi leo Jumamosi Oktoba 9,2021 cheti cha ushindi mshindi wa kiti cha udiwani katika kata ya Ndembezi Victor Thobias Mmanywa msimamizi wa uchaguzi huo kata ya Ndembezi Timothy Andrew Timoth amesema kuwa yeye kama msimamizi wa uchaguzi mdogo kata ya Ndembezi ameamua kumkabidhi cheti cha ushindi na kumtangaza rasmi Victor Thobias Mmanywa kuwa mshindi wan a fasi ya uchaguzi mdogo baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi huo.

Msimamizi huyo wa uchaguzi ameeleza kuwa hatua inayofuata baada ya kumkabidhi cheti cha ushindi Victor Thobias Mmanywa na kumtangaza kuwa diwani wa kata ya Ndembezi na kwamba hatua inayofuata diwani huyo atakwenda kuapishwa katika Baraza la madiwani la Manispaa ya Shinyanga tayari kuanza kutekeleza majukumu ya kuwakilisha wananchi wa kata ya Ndembezi.

Akipokea cheti cha uteuzi na kutangazwa rasmi kuwa Diwani wa kata ya Ndembezi Victor Thobias Mmanywa ameushukuru uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata na wilaya kwa kumuamini na kuahidi kufanya kazi kwa kuyaenzi yale yote ya yaliyoachwa na mtangulizi wake Hayati David Nkulila enzi za uhai wake.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Timothy Andrew Timothy (kushoto) akimtangaza na kumkabidhi cheti cha ushindi Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi Victor Thobias Mmanywa wa Chama Cha Mapinduzi kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa kuwania nafasi ya udiwani kata ya Ndembezi. Picha zote na Amos John
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Timothy Andrew Timothy (kushoto) akimtangaza na kumkabidhi cheti cha ushindi Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi Victor Thobias Mmanywa wa Chama Cha Mapinduzi kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa kuwania nafasi ya udiwani kata ya Ndembezi
Mhe. Victor Thobias Mmanywa (CCM) akizungumza baada ya kukabidhiwa cheti  na kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa kuwania nafasi ya udiwani kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Mhe. Victor Thobias Mmanywa (katikati) akifurahia baada ya kukabidhiwa cheti  cha ushindi na kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa kuwania nafasi ya udiwani kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga
Maandamano kuelekea nyumbani kwa Victor Thobias Mmanywa yakiendelea
Maandamano kuelekea nyumbani kwa Victor Thobias Mmanywa yakiendelea
Mhe. Victor Thobias Mmanywa (CCM) akizungumza nyumbani kwake baada ya kukabidhiwa cheti  na kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa kuwania nafasi ya udiwani kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga


Post a Comment

0 Comments