Header Ads Widget

ACT WAZALENDO WASHINDA UCHAGUZI JIMBO LA KONDE... MOHAMED SAID ISSA ATANGAZWA


Mgombe Ubunge Mohamed Said Issa kupitia Chama cha ACT Wazalendo ametangazwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo Konde kwa kupata kura 2391 huku mgombea wa CCM Mbarouk Amour Habib aliyepata kura 794 akifuatiwa na Salama Khamis Omar wa CUF aliyepata kura 98 na Hamad Khamis Mbarouk (AAFP) aliyepata kura 55 kati ya kura 3,338 zilizopigwa.

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Konde Abdallah Said Ahmed amemtangaza Mohamed Said Issa leo Jumamosi Oktoba 9, 2021 katika kituo cha majumuisho cha Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Post a Comment

0 Comments