Header Ads Widget

POSTA ARUSHA KUTOA MSAADA KWA WATOTO WALIOMAGEREZA ARUSHA.


Meneja wa Shirika la Posta,mkoa wa Arusha,Athman Msilikale akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya Siku ya Posta duniani,yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 9,2021.
 
Mwandishi wetu, Arusha

Shirika la Posta Tanzania,mkoa wa Arusha linatarajia kuwatembelea na kutoa misaada kwa watoto wenye uhitaji katika Gereza la watoto mkoa Arusha ikiwa ni maadhimisho ya siku ya posta Duniani.
Mbali ya kutoan misaada mbalimbali,shirika hilo linatarajia kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali linazotoa kwa wananchi katika maadhimisho hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 5,2021 ofisini kwake,Meneja wa Shirika hilo mkoa wa Arusha,Athman Msilikale,alisema maadhimisho hayo yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma,yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Ubunifu kwa Posta Endelevu”

Alisema shirika hilo mkoani hapa linatarajia kurejesha sehemu ya faida yake kwa jamii kwa kutembelea watoto hao wenye uhitaji Oktoba tisa mwaka huu,ili kuwafariji wasijione wametengwa na jamii.

“Tunaona ni vizuri kurejesha jamii kwa kutembelea watoto katika gereza hilo kuwafariji wasijione ni jamii iliyotengwa baada ya wazazi wao kuhukumiwa,kuwapa misaada kama sehemu ya jukumu la shirika na kuthibitisha ni mali ya serikali na ina jukumu la kuhudumia jamii,”

“Hili ni shirika la serikali,tunaona ni muhimu tuipeleke kwa wananchi kwa sababu tunaona ni vizuri tukashirikiana na wananchi kwa pamoja,”

“Kama sehemu ya jamii tunaenda kukutana na wale watoto kwa lengo la kuwafariji,kuwapa misaada midogo kulingana na mahitaji yao ,”aliongeza

Meneja huyo alisema mbali na kuungana na watoto hao,watatumia fursa hiyo kuelezea huduma zao za posta ambazo wamekuwa wakizifanya ikiwemo utumaji wa barua,nyaraka na vifurushi kupitia huduma ya EMS.

Alisema Shirika hilo la Kimataiafa lina Umoja wa Posta kuanzia kidunia,Afrika na Afrika Mashariki na tuna mtandao mkubwa kuliko mashirika mengine ambapo duniani kuna vituo vya kutoa huduma vinavyokaribia 600,000.

“Hivyo wananchi wa nchi moja hadi nyingine wanaweza kutumia shirika la posta kwa ajili hya kusafirisha vifurushi,barua na fedha kutoka nchi moja kwenda nyingine kirahisi kwa kutumia huu mtandao,”aliongeza Meneja


Meneja huyo alisema moja ya huduma mpya zilizozinduliwa hivi kaibuni ni pamoja na Huduma kwa pamoja (One stop Center),ambapo huduma mbalimbali za kiserikali zitakuwa zinapatika katika ofisi za Shirika hilo na zitamrahisishia mwananchi kupunguza mzunguko kwenda kwenye ofisi hizo.




Post a Comment

0 Comments