Header Ads Widget

DC MBONEKO AONGOZA WANANCHI KUCHIMBA MSINGI UBORESHAJI HUDUMA KITUO CHA AFYA SALAWE WILAYANI SHINYANGA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiongoza Wananchi wa Salawe kuchimba Msingi kujenga Jengo la wagonjwa wa nje (OPD)na Maabara katika kituo cha Afya Salawe wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ameongoza wananchi wa Salawe wilayani humo, kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wanje (OPD) na Maabara, ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
 
Zoezi la uchimbaji msingi limefanyika leo kwenye kituo hicho cha Afya Salawe, ambalo limehudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwamo wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Shinyanga.

Mboneko akizungumza na wananchi mara baada ya kumaliza kuchimba Msingi, amesema Rais Samia Suluhu Hassani, ametoa Sh. milioni 500 kwa ajili ya kuboresha kituo cha Afya Salawe wilayani Shinyanga, na Oldshinyanga Manispaa ya Shinyanga, ili kuboresha huduma za Afya kwa wananchi.

Alisema katika kituo hicho cha Afya Salawe, Rais Samia ametoa Sh. milioni 250, kwa ajili ya kujenga Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Maabara, pamoja na kichomea taka, na kubainisha kuwa hiyo ni hatua ya awali, ambapo Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya zaidi, ikiwamo upatikanaji wa Madawa ya kutosha na Madaktari.

“Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassani kutupatia fedha Sh.milioni 500, fedha ambazo zimepatikana kupitia Tozo ya miamala ya Simu, ambapo kwenye kituo hiki cha Afya Salawe tumepewa Sh. milioni 250, hivyo hivyo na kituo cha Afya Oldshinyanga, ambapo tunajenga jengo la wagonjwa wanje, maabara, na kichomea taka,”alisema Mboneko.

“Nasisi kama Serikali Shinyanga, tutaendelea kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato, ili kuendelea kuunga juhudi za Rais wetu katika kuhudumia wananchi, ambapo tutaendelea pia na uboreshaji wa majengo katika vituo vya afya, na wananchi kupata huduma bora na kuimarisha afya zao,”aliongeza.

Katika hatua nyingine aliwataka wananchi wa Salawe, wakitumie kituo hicho cha Afya kupata huduma za matibabu, na siyo kwenda kwa waganga wa kienyeji, sehemu ambayo hawawezi kupata huduma stahiki, zaidi ya kuharibu afya zao na hata kupoteza maisha.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Dk. Mameritha Basike, alisema kituo hicho cha Afya Salawe hakina chumba cha upasuaji wala wodi ya wazazi, lakini utolewaji wa fedha hizo na Rais Samia, utasaidia kupunguza changamoto hiyo, pamoja na wananchi kutofuata huduma za Afya umbali mrefu zaidi ya Kilomita 70 kwenda Hospitali ya wilaya.

Nao Baadhi ya Akina mama wa Salawe ambao walijitokeza kuchimba Msingi akiwamo Doricas Evarist na Modesta Charles, wamempongeza Rais Samia, pamoja na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwa kujali Afya za wananchi na kuwaboreshea huduma za Afya.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiongoza Wananchi wa Salawe kuchimba Msingi kujenga Jengo la wagonjwa wa nje (OPD)na Maabara katika kituo cha Afya Salawe wilayani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiongoza Wananchi wa Salawe kuchimba Msingi kujenga Jengo la wagonjwa wa nje (OPD)na Maabara katika kituo cha Afya Salawe wilayani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiongoza Wananchi wa Salawe kuchimba Msingi kujenga Jengo la wagonjwa wa nje (OPD)na Maabara katika kituo cha Afya Salawe wilayani Shinyanga, kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Emmanuel Lukanda.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiongoza Wananchi wa Salawe kuchimba Msingi kujenga Jengo la wagonjwa wa nje (OPD)na Maabara katika kituo cha Afya Salawe wilayani Shinyanga, kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mameritha Basike.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) akiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Ernestina Richard wakiwa wamebeba Mbao.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Ernestina Richard, akishirikiana na Wananchi wa Salawe kuchimba Msingi.

Katibu wa itikadi na Uenezi wilaya ya Shinyanga Emmanuel Lukanda, akichimba Msingi.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga Abdala Kilobi akichimba Msingi.

Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja akichimba Msingi.

Mganga Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Dk. Mameritha Basike, (kulia) akichimba Msingi.

Wananchi wa Salawe wilayani Shinyanga wakichimba Msingi kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na Maabara kwa ajili ya kuboresha huduma kituo cha Afya Salawe.

Wananchi wa Salawe wilayani Shinyanga wakichimba Msingi kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), na Maabara kwa ajili ya kuboresha huduma kituo cha Afya Salawe.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments