Header Ads Widget

CHEREHANI ATANGAZWA RASMI KUWA MBUNGE MTEULE JIMBO LA USHETU


Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ushetu Mkoa wa Shinyanga Bw. Linno Mwageni amemtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Emmanuel Peter Cherehani kuwa Mbunge Mteule wa Jimbo hilo.
 
Katika uchaguzi huo uliofanyika jana Oktoba 9, 2021 Cherehani alipata kura 103,357 dhidi ya mshindani wake Bw. Mabula Nkwabi Julius wa ACT Wazalendo aliyepata kura 3,588 kati ya kura 106,945 zilizopigwa.

Uchaguzi huo umefanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Elias John Kwandikwa ambaye pia alikuwa Waziri wa Ulinzi kufariki Agosti 2, 2021.

●Idadi ya wapiga kura walioandikishwa.165418

●Idadi ya waliopiga kura 107188

●Idadi ya kura halali 106945

●Idadi ya kura zilizokataliwa 243

●ACT Wazalendo 3588 (3.4%)

●Chama cha Mapinduzi (CCM) 103357. (96.6%)

Post a Comment

0 Comments