CCM YAKEMEA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO, MAADHIMISHO JUMUIYA YA WAZAZI
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anold Makombe, amekemea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, huku akisisitiza kudumisha amani ya nchi.
Amebainisha hayo leo Mei 9, 2026 alipokuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 71 ya Jumuiya ya Wazazi, yaliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Galamba, Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Amesema kwa sasa kumekithiri tatizo la mmomonyoko wa maadili, hivyo ni vyema watu wakawa na umoja, amani na upendo na kuacha kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili.
Aidha, amewataka pia wananchi waendelee kudumisha amani ya nchi.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Dorisi Kibabi, amesema katika maadhimisho hayo, wametoa elimu ya malezi bora kwa watoto, kufanya matendo ya huruma, kutembelea wagonjwa na kuwapatia sabuni na mafuta.
Amesema pia wametoa chakula kwa watoto shuleni pamoja na kupanda miti 361 kwa ajili ya kutunza mazingira.
VIDEO CHINI YA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe akizungumza.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha akizungumza.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini Fuel Mlindoko akizungumza.
Katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini Dorisi Kibabi akizungumza.
Katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini Doris Kibabi akizungumza.
Diwani wa Kolandoto Mshagatila Moses akizungumza.
VIDEO
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464