Header Ads Widget

OPE WATAMBULISHA KILIMO CHA MTAMA WILAYANI SHINYANGA KUMKOMBOA MKULIMA

Mkurugenzi wa Shirika la Organization of People Empowerment (OPE) la mkoani Shinyanga Bwana William Shayo, wakati wa kutambulisha mradi wao wa Kilimo cha Mtama wilayani Shinyanga.


Na Josephine Charles

SHINYANGA.

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga hususani wa Kata za Mwalukwa na Pandagichiza, wametakiwa kuunga mkono mradi wa kilimo cha Mtama, ili kupata mavuno mengi na kukabiliana na tatizo la njaa na kuwainua kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa Shirika la Organization of People Empowerment (OPE) la mkoani Shinyanga Bwana William Shayo, baada ya kuzindua na kutambulisha mradi huo kwa viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwemo maafisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri hiyo, pamoja na maafisa kilimo wa Kata za Pandagichiza na Mwalukwa, ambapo mradi utatekelezwa kwenye vijiji nane.

Amesema lengo la mradi huo ni kuwajengea uwezo wakulima hasa makundi ya akina mama wanaojishughulisha na kilimo cha Mtama, ili waweze kuzalisha kwa tija zaidi pamoja na kuhakikisha uzalishaji wa sasa wa Tani 1.28 unapanda hadi Tani 2.28 ili pia waweze kuhudumia familia zao pamoja na kujiongezea kipato.

Mkurugenzi huyo amesema mradi huo ni sehemu ya mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya mama na mtoto (MTAKUWWA) au NPA kwa maana ya kuwajengea uwezo wa kiuchumia kina mama.

Kwa upande wao Maafisa kilimo kutoka kata za Pandagichiza na Mwalukwa akiwamo Eda Kurume, wamesema mradi huo wameupokea na utatekelezwa vizuri, kwa sababu zao la mkakati katika kata hizo ni Mtama,hivyo wamesema kwa kuwa watabiri wa hali ya hewa mwaka huu, wamesema kutakuwa na mvua chache, hivyo wataenda kuhamasisha kilimo cha zao hilo kwa kuwa ni moja kati ya zao linalostahimili ukame.

Awali mradi huu ulianzia Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa wakulima waliacha kutumia njia za kawaida, na badala yake walitumia njia za kisasa za kilimo hicho,  na ndiyo maana wameamua kuendeleza mradi huo wa kilimo cha Mtama kwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.


Mkurugenzi wa Shirika la Organization of People Empowerment (OPE) la mkoani Shinyanga Bwana William Shayo, wakati wa kutambulisha mradi wao wa Kilimo cha Mtama wilayani Shinyanga.

Maofisa maendeleo na ugani wakiwa kwenye utambulisho wa mradi wa kilimo cha Mtama wilayani humo.

utambulisho wa mradi ukiendelea.

utambulisho wa mradi ukiendelea.


Post a Comment

0 Comments