Header Ads Widget

WADAU WAIOMBA SERIKALI KURIDHIA MKATABA WA KIMATAIFA WA HAKI ZA WAFANYAKAZI WA NDANI

Wadau mbalimbali wa haki za watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika leo kwenye uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela.

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Serikali imeombwa kulidhia mkataba namba 189 wa kimataifa wa haki za wafanyakazi wa ndani ili waweze kufanya kazi za staha na kupata stahiki zao kwa wakati.

Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kutetea haki za Wafanyakazi wa Nyumbani la WoteSawa, Angela Benedicto kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kwenye uwanja wa Furahisha uliopo wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.

Alisema wakati wakiadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16, pia ni siku ambayo tunakumbukia Shirika la kazi Duniani (ILO)pamoja na wanachama wake Nchini Geniva lilisaini mkataba wa wafanyakazi wa Nyumbani.

"Tunaomba Serikali iweze kulidhia mkataba huo kwa sababu ni daraja kubwa kwa wadau na wafanyakazi ili waweze kufanya kazi zao kwakuwa na uhakika wa kupata mishahara yao kwa wakati na tunaendelea kuhamasisha waajiri kuwalinda wafanyakazi hao ili wasitendewe ukatili kwani ukimlinda na kumpenda familia yako pia itakuwa salama",alisema Angela.

Aidha alisema kuwa Serikali na wadau waendelee kutekeleza na kusimamia Sheria na miongozo iliyopo Nchini ili waweze kuwalinda Watoto dhidi ya vitendo vya ukatili, aliongeza kuwa Shirika hilo tangu mwaka 2012 limeokoa Watoto 6,00 waliofanyiwa vitendo vya ukatili nakufanikiwa kuwarundisha kwao.

Meneja wa Shirika la Sos Children Village Mwanza, Dorothy Ndege alisema wanaofanya kazi kwa ukaribu na Serikali kwenye miradi yao na kwa nusu Mwaka wametumia zaidi ya million 100 kwa ajili ya miradi ya Elimu na Afya ili kupunguza changamoto zinazowakabili Watoto kwenye mahitaji yao muhimu.

Alisema pamoja na juhudi zinazofanywa na asasi mbalimbali za kuwalinda na kuwatetea Watoto hao wanatakiwa kupaza sauti zao ili waweze kujilinda wenyewe Hali itakayosaidia kufikia malengo na kutimiza ndo to zao.

Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk. Severine Lalika aliezungumza kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabliel ameitaka Jamii kufichua wazazi na walezi wanaotenda vitendo vya ukatili kwa Watoto wao ili wachukuliwe hatua za kisheria kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza au kumaliza kabisa ukatili katika Jamii.

Maadhimisho hayo yalibeba kaulimbiu isemayo "Tutekeleze Ajenda 2040: kwa Afrika inayolinda haki za Mtoto"


Post a Comment

0 Comments