Header Ads Widget

WANANDOA WILAYANI KISHAPU WAFARIKI KWA KUJICHOMA MOTO KWA MADAI YA BIBI HARUSI KUKATALIWA UKWENI

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, Jackson Mwakagonda

Wanandoa wawili ambao ni Wenslausi James (30) na Betha Kasimili (25), ambao ni wakazi wa Kijiji cha Busongo Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, wamefariki dunia baada ya kujilipua moto kwa kutumia Mafuta ya Petrol, kwa madai ya wazazi wa mwanaume kumkataa mwanamke.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, Kamishina msaidizi wa Polisi, Jackson Mwakagonda, akitoa taarifa leo kwa vyombo vya habari, amesema tukio hilo limetokea June 14 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi.

Alisema wanandoa hao walikuwa wamezaa watoto watatu, lakini wazazi wa mwanaume walimkataa mkewake, na kuamua kuuvunja mji pamoja na kurudisha Mahali nyumbani kwao na mwanamke.

Aidha amesema baada ya mji huo kuvunjika, ndipo mwanaume akasikia kuwa mkewake anataka kuolewa, na kuamua kwenda kwao na mwanamke akiwa na dumu la mafuta ya Petrol lita tano,na kisha kuingia chumbani kwa mwanamke na kufunga mlango na kuanza kugombana.

"Mwanaume huyu alimchoma kisu cha ubavuni mkewake, na kisha kumfunga minyororo na kumwagia mafuta ya Petrol, kisha na yeye kujimwagia Petrol akawasha kiberiti na kujilipua moto, ambapo waliteketea pamoja na nyumba," alisema Mwakagonda.

Aidha Kamanda ametoa wito kwa wazazi, kuacha kuingilia ndoa za watoto wao, pamoja na wanandoa kuacha kujichukulia sheria Mkononi, na pale penye migogoro bali watafute ufumbuzi kwa kufuata sheria.


Post a Comment

0 Comments