Header Ads Widget

MADIWANI MANISPAA SHINYANGA WAJADILI HOJA ZA CAG, DC MBONEKO AWACHARUKIA WATENDAJI


Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wakipitia Makabrasha yenye taarifa za hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG).

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wamejadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) katika mwaka wa fedha 2019-2020.

Kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa hiyo ya CAG, kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa hiyo na kuhudhuriwa na watalaam, viongozi wa kisiasa na baadhi ya wananchi.

Akisoma taarifa ya CAG kwenye baraza hilo maalum la madiwani Manispaa ya Shinyanga, Mweka hazina wa Manispaa hiyo, Nickson Itogoro, alisema kwa kipindi cha kuanzia Juni 30 mwaka 2020 halmashauri hiyo imepata hati Safi, lakini zimeibuliwa hoja 67.

Alisema kati ya hoja hizo 67, hoja 26 ni za kipindi cha nyuma, lakini hoja 41 ni za kipindi cha kuanzia Juni 30 mwaka jana, huku akibainisha kuwa mpaka sasa zimeshajibiwa hoja 25 na kubaki 42 ambazo bado zinaendelea kujibiwa.

Akizungumza kwenye baraza hilo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, ameagiza wataalam wa Manispaa ya Shinyanga ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa uzembe na kusababisha kuwapo na hoja hizo za CAG wachukuliwe hatua.

“Hoja ambazo zimetolewa na CAG naziona kabisa zinatokana na uzembe, haiwezekani mtu unakaa na fedha za mapato ya Serikali mfuko hata ndani ya mwezi mmoja na kutozipeleka benki, pamoja na fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo kutopelekwa kwenye maeneo husika, huu ni uzembe,” amesema Mboneko,

“Ifike mahala watu ambao wanatusababishia hoja hizi za CAG wachukuliwe hatua, sababu ukiangalia baadhi ya hoja zinajirudia rudia kila mwaka, na hili katika mwaka wa fedha ujao sitaki kuona linajirudia,”ameongeza.

Naye Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Serikali za mitaa Mkoani Shinyanga, Alphonce Kasamji, amesema siri ya mfanikio ya halmashauri kupata hati Safi ni kujibu hoja za CAG kwa wakati na kutokuwa na hoja nyingi, pamoja na Wataalam kushirikiana kiutendaji na wakaguzi wa ndani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyangta Geofrey Mwangulumbi, alisema katika hoja ambazo zimetolewa na CAG, Halmashauri hiyo ndiyo ina hoja chache, huku akiahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote ambayo yametolewa kwenye baraza hilo.

Aidha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, David Nkulila, amewata pia wakuu wa Idara wa Manispaa hiyo wakae mguu sawa, kwa kuhakikisha wanatoa taarifa na kufuta hoja zote za CAG kila mmoja kwenye eneo lake.

Nao baadhi ya Madiwani wa Manispaa hiyo akiwamo Ezekiel Sabo wa Ibinzamata, walisema changamoto zote za kiutendaji ambazo zimejitokeza katika mwaka wa fedha 2019-2020, na kusababisha kuwapo na hoja hizo za CAG zifanyiwe kazi ili Halmashauri hiyo iendelee kulinda heshima yake ya kupata Hati Safi, na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Baraza hilo maalum la Madiwani Manispaa ya Shinyanga lililokuwa na Ajenda moja ya kujadili taarifa ya CAG na kufuta hoja zilizotolewa.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga Alphonce Kasanji, akizungumza kwenye Baraza hilo maalumu la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, akizungumza kwenye kikao cha Baraza maalum la madiwani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akizungumza kwenye Baraza hilo.
Mwekahazina wa Manispaa ya Shinyanga Nickson Itogoro, akisoma taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa, kwenye Baraza Maalum la Madiwani.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye Baraza maalum la kujadili Taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye Baraza maalum la kujadili Taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye Baraza maalum la kujadili Taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye Baraza maalum la kujadili Taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.

Wataalam wa manispaa ya Shinyanga ,wakiwa kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Wataalam wa manispaa ya Shinyanga ,wakiwa kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Wataalam wa manispaa ya Shinyanga ,wakiwa kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa .


Post a Comment

0 Comments