Header Ads Widget

WAZIRI BASHUNGWA AAGIZA MASHABIKI 43,947 WAREJESHEWE TIKETI, MCHEZO SIMBA VS YANGA KUPANGWA UPYA


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ameagiza mashabiki 43,947 waliokata tiketi kwenye mchezo wa Simba SC na Yanga SC kurejeshewa tiketi zao kwenye mfumo wa kadi za kuingilia uwanjani ili tiketi hizo hizo ziwasaidie kuingia uwanjani na kukaa eneo lile lile alilokaa awali siku na tarehe itakayopangwa kurudiwa mechi hiyo iliyoahirishwa.

Aidha, amesema mfumo huo uwaruhusu mashabiki wengine ambao awali hawakukata tiketi waweze kukata tiketi za mchezo huo endapo watataka na kukidhi idadi inayoruhusiwa kulingana na uwezo wa uwanja.

Maamuzi hayo yametokana na kikao cha pamoja kilichofanyika kati ya wizara hiyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi, Baraza la Michezo Tanzania na klabu za Simba na Yanga.

Maelekezo ya Serikali juu ya hatima ya mechi iliyoahirishwa ya Yanga SC na Simba SC Mei 8, 2021.
1. Mechi itarudiwa (kwa tarehe itakayopangwa.
2. Mashabaki waliolipia kurejeshewa tiketi upya ili waweze kuingia uwanjani
3. Ruksa kwa mashabiki wapya kununua tiketi za kuuona mchezo huo.

Post a Comment

0 Comments