Header Ads Widget

MABADILIKO MENGINE YA WAKUU WA MIKOA LEO, NI KAFULILA NA MONGELLA

Mkuu mpya wa mkoa wa Arusha, John V. Mongella

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya safu ya wakuu wa mikoa miwili ya Arusha na Simiyu.

Mabadiliko hayo ni kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, John V. Mongella ambaye amebadilishwa kwenda mkoa wa Arusha, huku aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, David Kafulila akipelekwa Simiyu.

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo leo baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wapya wa mikoa na wakuu wa taasisi mbalimbali aliowateua Mei 15, mwaka huu.

Katika uteuzi huo wa Mei 15, mwaka huu, John Mongella aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alipelekwa Simiyu, huku Kafulila aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, akiteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha.

"Kuna jambo nilitaka niliseme, nimefanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa, John Mongella kwa sababu umetoka Mwanza na Mwanza ni jiji kubwa basi nakupeleka Arusha, wewe Kafulila kwa sababu ndiyo kwanza unaanza umetoka kuwa RAS basi nakupeleka Simiyu," amesema Rais.
Mkuu mpya wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila


Post a Comment

0 Comments