Header Ads Widget

FISI WAVAMIA MAKAZI YA WATU LUBAGA-SHINYANGA NA KUUA MBUZI 17,

Mbuzi na nyama ya mifugo waliouliwa na fisi katika mtaa wa Azimio Kata ya Lubaga mjini Shinyanga wakiteketezwa

Na Mwandishi wetu, Shinyanga
Wakazi wa Mtaa wa Azimio Kata ya Lubaga katika Manispaa ya Shinyanga wameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto ya uwepo wa fisi kwenye maeneo yao baada ya fisi kuvamia zizi na kuua mbuzi 17 wa familia ya Monica Paul mkazi wa eneo hilo.

Wakizungumzia tukio hilo wakazi wa kata ya Lubaga wamesema kuwa kwa sasa fisi hao wamekuwa wakionekana marakwamara katika maeneo yao tofauti na ilivyo kuwa siku za nyuma ambapo fisi hao usiku wakuamkia leo wamevamia katika familia hiyo na kuua mbuzi pamoja na kondoo katika familia hiyo.

Aidha wakazi wa Kata hiyo akiwemo diwani wakata ya Lubaga Reuben Dotto wameeleza kuwa changamoto ya uwepowa fisi kwenye maeneo yao imesababisha hofu kwa wakazi wakata hiyo na kupelekea baadhi ya wanafunzi kushindwa kuudhuria shuleni mapema wakihofia kuumwa na fisi.

Kwa upande wao ndugu wafamilia ya Paul wameongeza kuwa ilikuwa majira ya saa kumi usiku ndipo waliposikia mlio wa fisi hali iliyo walazimu kutoka nje na baada ya kutoka nje ndipo walipo gundua kuwa mbuzi wao wamekwishauliwa na fisi.

Naye Afisa Mifugo Kata ya Lubaga, Eliaremisa Mbise amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwaamrisha wakazi wakata hiyo kuteketeza masalia ya mbuzi walio uliwa na fisi kwa moto ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kula nyama ya mifugo waliouliwa na fisi.
Diwani wa Kata ya Lubaga, Reuben Dotto (kulia) akiwajulia hali familia ya Monical Paul na kujionea namna mifugo ya familia hiyo ilivyouliwa na Fisi
Afisa Mifugo wa kata ya Lubaga akifanya uchunguzi kwenye mifugo iliyouawa na Fisi ili kuiteketeza
Wananchi wa eneo hilo wakiipa faraja familia iliyokumbwa na mkasa huo



Post a Comment

0 Comments