Header Ads Widget

SIDO SHINYANGA YAWAITA WAJASIRIAMALI KUPATA MIKOPO, UJUZI NA TEKNOLOJIA YA VIWANDA...SH. MILIONI 80 ZAKOPESHWA KWA WAJASIRIAMALI 125

Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Kweka akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake mjini Shinyanga

Na Damian Masyenene, Shinyanga
ILI kuhakikisha huduma zinazotolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa Shinyanga ikiwemo uendelezaji wa teknolojia kuboresha bidhaa mbalimbali, fedha na mitaji, Habari na masoko zinawafikia wajasiriamali wengi na kuondoa utegemezi na tatizo la ajira, Shirika hilo limewahimiza wananchi kujitokeza kupata mikopo, ujuzi, mafunzo na teknolojia mbalimbali za viwanda ikiwemo mashine.

Wito huo umetolewa leo Aprili 27, 2021 na Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga, Hopeness E. Kweka wakati akizungumza na Shinyanga Press Club Blog ofisini kwake, ambapo ameeleza kuwa zaidi ya Sh. Milioni 800 zimetengwa kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali mbalimbali mkoani humo.

Kweka ameeleza kuwa kwa kipindi cha miezi sita (Desemba 2020 hadi Machi, 2021), SIDO Shinyanga imekopesha jumla ya wajasiriamali 125 kiasi cha Sh Milioni 80 hadi 90 kwa ajili ya kuongeza ufanisi na ubora kwenye bidhaa zao na kutunisha mitaji yao.

Pia wametoa elimu kwa wajasiriamali ili kuboresha bidhaa zinazokidhi viwango vya TBS na TMDA, namna ya kukokotoa mahesabu, ambapo wajasiriamali 80 walifikiwa na elimu hiyo na 35 kupata mikopo Manispaa ya Kahama, 54 wakapata mikopo manispaa ya Shinyanga na 47 kutoka wilaya ya Kishapu wakapata mafunzo ya uboreshaji bidhaa, vifungashio na kuweka lebo.

Amesema kuwa wanatoa mikopo ya Sh Milioni 1 hadi 6.5 kwa wajasiriamali wadogo na Sh Milioni 8 hadi 500 kwa wajasiriamali wakubwa (mikopo mikubwa).

Hata hivyo, Kweka ameeleza kuwa licha ya jitihada hizo za kuwawezesha wajasiriamali, bado mwitikio wa wananchi ni mdogo na hawajitokezi kuchangamkia fursa pale huduma kutoka Sido zinapotangazwa.

“Tunazo program za vijana ikiwemo Kitamizi ambayo tunawawezesha wenye mawazo ya kijasiriamali, pia vijana baada ya shule na ujasiriamali ambayo tunawakaribisha waliomaliza shule lakini hawana namna ya kupata ajira, tunawaalika vijana waje wapate ujuzi, uwezeshaji, mikopo na teknolojia kutoka kwetu ili waanzishe biashara zao,” amesema.

Mbali na mikopo na ujuzi, Meneja Kweka ameeleza kuwa wanacho kituo kikubwa cha kuendeleza teknolojia ambacho kinazalisha mashine mbalimbali kwa ajili ya wajasiriamali kutoka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa na mikoa mingine Jirani.

Ameongeza kwa kueleza kuwa kituo hicho kimeweza kuzalisha teknolojia ya kuchakata mazao ya kilimo na mifugo Pamoja na teknolojia ya vifaa vya ujenzi, ambazo ndizo zimekuwa na soko kubwa katika ukanda huo hususan mkoa wa Shinyanga.

“Teknolojia tunayotoa tumezingatia mazingira yetu kwahiyo teknolojia yetu ni rafiki, wanaopata teknolojia wanapata pia mafunzo na kuelekezwa namna ya kutumia na teknlojia yetu inapatikana kwa bei Rafiki. Vile vile, tunatoa mashine hizi kwa mkopo,” amebainisha.
Meneja wa SIDO-Shinyanga, Hopeness Kweka akizungumzia mikakati mbalimbali ya shirika hilo na namna linavyowawezesha wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa kwa njia ya mikopo ya mitaji na teknolojia
Meneja wa SIDO -Shinyanga (Kulia) akielezea namna kituo cha kuendeleza teknolojia kinavyofanya kazi ya kuzalisha mashine mbalimbali ambazo huuzwa ama kukopeshwa kwa wajasiriamali
Meneja huyo akionyesha mashine ya kuchakata ngozi
Akionyesha mashine ya kukata bidhaa mbalimbali za ngozi


Kweka akionyesha baadhi ya mashine zinazozalishwa na zinazopatikana kwenye kituo cha kuendeleza teknolojia kilichopo SIDO Shinyanga eneo la Ibinzamata
Mitambo na mashine mbalimbali zinazopatikana katika kituo cha kuendeleza teknlojia Kilichopo SIDO Shinyanga -Ibinzamata

Hii ni mashine ya kuosha viazi ambayo imetengenezwa na SIDO katika kituo chao cha kuendeleza teknolojia. Ambapo Meneja wa Sido Shinyanga, Hopeness Kweka (aliyevaa shati jeupe) akifafanua namna inavyofanya kazi
Meneja huyo akionyesha mashine ya kusaga ambayo imetengenezwa na SIDO Shinyanga katika kituo chao cha kuendeleza teknolojia
Kifaa cha kukausha viazi ambacho kimetengezwa na SIDO Shinyanga





Post a Comment

0 Comments