Header Ads Widget

MCHUNGAJI KANUNU ATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM BUHANGIJA




Mchungaji wa Kanisa la Baptist Nyanhende Manispaa ya Shinyanga, Renatus Kanunu, akiwakabidhi msaada wa vitu mbalimbali kikiwemo Chakula, watoto wenye mahitaji maalumu wanaolelewa kituo cha Buhangija.

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mchungaji wa Kanisa la Baptist lililopo Nyanhende Manispaa ya Shinyanga, Renatus Kanunu, ametoa msaada wa vitu mbalimbali kikiwamo chakula, kwa watoto wenye mahitaji maalumu, ambao wanalelewa katika kituo jumuishi cha Buhangija.

Msaada uliotolewa na mchungaji huyo ni Kilo 200 za Mchele, Sabuni za unga Kilo 30, Kilo 150 za Unga wa Sembe, Dagaa debe Mbili, Maharage Kilo 40, Mafuta ya kupikia ndoo moja, Biskuti, Vikombe 240, mifagio, stili waya na mipira miwili ya kuchezea kwa wasichana na wavulana.

Kanunu amekabidhi msaada huo leo na kueleza kuwa jamii inapaswa kuguswa kusaidia watoto hao ili kuwaondolea changamoto ambazo zinawakabili.

Amesema kuwa, kama mchungaji ameguswa na watoto hao wenye mahitaji maalumu, na amekuwa akitoa msaada kila mara na sasa anaendelea na utamaduni huo, ili kuwapa faraja watoto hao pamoja na kutimiza ndoto zao kama watoto wengine.

Pia amewataka watoto hao wasome kwa bidii iliwatimize ndoto zao, pamoja na kupendana wao kwa wao,ikiwamo na kizingatia masharti ya wataalamu wa afya kwa kunawa mikono mara kwa mara ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko hasa kipindupindu na Corona.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya kituo, Mlezi Msaidizi wa kituo hicho, Loyce Daudi, amesema msaada huo wamepewa wakati muafaka, kwani walikuwa na uhitaji nao kutokana na baadhi ya wazazi wa watoto hao kuwatelekeza kituoni hapo na hakuna msaada wowote kutoka kwao.

Aidha amesema kitu hicho cha Buhangija jumuishi, hua kinalea watoto wenye ualbino, usikivu na uoni hafifu, ambapo jumla yao wapo 213 na kipo chini ya Serikali, lakini baadhi ya mahitaji hayatolewi na Serikali na wanaishi kwa kutegemea wadau.

Nao baadhi ya watoto hao wenye mahitaji maalumu akiwamo Paschal Juma, wameshukuru kupewa msaada huo, na kutoa wito kwa wadau wengine waendelee kuwasaidia.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mchungaji wa Kanisa la Baptist la Nyanhende Manispaa ya Shinyanga, Renatus Kanunu (Katikati) akizungumza kabla ya kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu ambao wanalelewa katika kituo cha Buhangija jumuishi.
Mchungaji Renatus Kanunu, akitoa nasaha kwa watoto wenye mahitaji maalumu ambao wanalelewa kwenye kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Mlezi msaidizi wa kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija, Loyce Daudi akitoa shukrani ya msaada huo kwa niaba ya watoto hao wenye mahitaji Maalumu.
Mchungaji wa Kanisa la Baptist Nyanhende Manispaa ya Shinyanga, Renatus Kanunu, akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu wanaolelewa kituo cha Buhangija kikiwamo Chakula.
Mchungaji wa Baptist Renatus Kanunu, kushoto, akikabidhi msaada katika kituo cha kulea watoto wenye Mahitaji maalumu Buhangija.
Mchungaji wa Baptist Renatus Kanunu, kushoto, akikabidhi mipira miwili kwa ajili ya michezo kwa watoto hao wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija.
Muonekano wa vitu vya msaada.
Mchungaji wa Kanisa la Baptist la Nyanhende Manispaa ya Shinyanga Renatus Kanunu, akigawa Biskuti kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija.
Watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija, wakiwa kwenye zoezi la kupewa msaada wa vitu mbalimbali na Mchungaji wa Kanisa la Baptist la Nyanhende Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija, wakiwa kwenye zoezi la kupewa msaada wa vitu mbalimbali na Mchungaji wa Kanisa la Baptist la Nyanhende Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha Buhangija, wakiwa kwenye zoezi la kupewa msaada wa vitu mbalimbali na Mchungaji wa Kanisa la Baptist la Nyanhende Manispaa ya Shinyanga.


Post a Comment

0 Comments