Header Ads Widget

MWILI WA MKURUGENZI MTENDAJI SHUWASA WAAGWA SHINYANGA, SPC, WADAU WASHIRIKI...KUZIKWA KESHO MWANZA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga (Picha na Kadama Malunde).

Na Shinyanga Press Club Blog
Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) umewasili leo mjini hapa na kuagwa na mamia ya waombelezeaji, wadau mbalimbali wa maendeleo na baadhi ya wawakilishi wa taasisi mbalimbali ikiwemo Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).

Flaviana Kifizi (40) alifariki dunia jana Aprili 20,2021 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam akiumwa kichwa.

Shughuli ya kuaga mwili huo imefanyika leo nyumbani kwake Lubaga Mjini Shinyanga, ambapo Marehemu ameacha mtoto mmoja wa kike.

Akitoa salamu za Serikali ya Mkoa wa Shinyanga, Katibu Tawala Mkoa wa huo, Albert Msovela amesema Flaviana alijituma na kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha wananchi wa Shinyanga wanapata huduma ya maji safi na salama.

“Taarifa za kifo cha Flaviana zimetushtua sana kama mkoa. Niwaambie tu kuwa hakuna kazi ngumu kama kuwa kiongozi wa taasisi inayohusika kwa sababu maji hayana mbadala. Flaviana alitamani kila eneo, kila uchochoro wa Shinyanga upate huduma ya maji. Tumefanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha wananchi wa Shinyanga wanapata maji”,amesema Msovela ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa SHUWASA.

“Flaviana alikuwa msimamizi mzuri na kiungo mzuri katika mkoa wa Shinyanga. Alikuwa msikivu na alipenda kuwa na maamuzi ya pamoja na ndiyo maana SHUWASA imekuwa ikifanya vizuri na imeendelea kukua. Naomba tuenzi mambo aliyoyasimamia na kuyaanzisha na alitamani yafanyike”,ameongeza Msovela.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amesema Flaviana hakubagua watu na alikuwa rafiki wa kila mtu na alitimiza wajibu wake kikamilifu na kuipa sifa nzuri SHUWASA kwa kujali wananchi.

“Kifo cha Flaviana ni pigo kwetu serikali na wananchi kwa ujumla. Flaviana alishirikiana na viongozi wa serikali na wadau katika kuwapatia huduma ya maji wananchi. Hata kama kazi ilikuwa ngumu ukimuagiza kufanya yeye alifanya. Mama yake na Flaviana ni Jasinta na mimi naitwa Jasinta, alikuwa ananiita mama. Naomba tumuenzi kwa mazuri aliyofanya”,amesema Mboneko.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Mwamvua Jilumbi amemwelezea Flaviana kuwa alikuwa kiongozi Jembe aliyefanikiwa kujenga misingi imara SHUWASA hivyo watamkumbuka kutokana na usikivu,utendaji kazi na bidii yake katika kazi.

“Flaviana alipenda sana kazi yake. Hakuwa Mhandisi lakini alikuwa anafanya kazi kama amesomea uhandisi. Ameitumikia SHUWASA kwa zaidi ya miaka 10 mwanzo akiwa Meneja wa Rasilimali na utawala kisha Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA”,ameongeza Jilumbi.

Mazishi ya mwili wa marehemu Flaviana Kifizi yanatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa Aprili 23,2021 jijini Mwanza.

TAZAMA PICHA HAPA
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) akimfariji mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo wakati wa zoezi la kuaga mwili wa Mkurugenzi huyo.


Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akitoa salamu za rambirambi wakati akiongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwakilishi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Sam Bahari akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Flaviana Kifizi
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akitoa salamu za rambirambi wakati akiongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akitoa salamu za rambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Mwamvua Jilumbi akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Parokia ya Lubaga, Philemon Chikala akiongoza Ibada ya Kumuombea mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Mwamvua Jilumbi (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko
Afisa Habari wa KASHWASA, Dkt. Mwidima Peter akitoa mwongozo wa kuaga mwili wa marehemu Flaviana Kifizi
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akifuta machozi wakati akiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Waombolezaji wakiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mjumbe wa Kamati tendaji ya SPC, Marco Maduhu (wa pili kutoka kulia) na Mwanachama wa klabu hiyo, Sam Bahari (wa tatu kutoka kulia) wakiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Estomine Henry (wa pili kulia) na Mjumbe wa kamati tendaji ya Klabu hiyo, Frank Mshana (wa kwanza kulia) wakishiriki kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mjumbe wa Kamati tendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Suzy Butondo (wa pili kutoka kulia) akishiriki kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Waombolezaji wakiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Waombolezaji wakiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka za maji nchini akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Meneja wa RUWASA mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Kayovela akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1Blog


Post a Comment

0 Comments