Header Ads Widget

WANAFUNZI LITTLE TREASURE WAMUOMBA RAIS SAMIA SULUHU KUISIMAMIA VYEMA SEKTA YA ELIMU


Mwanafunzi Comfort Pius anayesoma darasa la sita katika shule ya Msingi Little Treasure mkoani Shinyanga, akisaini kitabu cha maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WANAFUNZI wa shule ya Msingi na Sekondari Little Treasure mkoani Shinyanga, wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassani, kusimamia sekta ya elimu bure, pamoja na kuboresha miundombinu ya shule.

Wamesema hayo leo wakati walipofika kutia saini kitabu cha maombolezo kifo cha hayati Rais John Magufuli, katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kilichotokea Machi 17 mwaka huu.

Mmoja wa wanafunzi hao, Comfort Pius anayesoma darasa la sita katika shule hiyo, alisema watamkumbuka hayati Rais John Magufuli katika mchango wake mkubwa wa elimu, hasa katika suala la utoaji elimu bure, na uboreshaji wa miundombinu.

"Tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassani kuendeleza yale ambayo ameyaacha hayati Rais John Magufuli, kwa kutoa elimu bure pamoja na kuboresha miundombinu ya shule, ili tutimize ndoto zetu," alisema Pius.

Naye Mwanafunzi Janety Anthony anayesoma kidato cha tatu katika Shule hiyo ,alisema utoaji wa elimu bure imesaidia wanafunzi wengi ambao wazazi wao wasiokuwa na uwezo kwenda shule na kutimiza malengo yao.

Aidha Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Paulo John, alisema watamkumbuka hayati Rais John Magufuli, katika mchango wake mkubwa kwenye sekta ya elimu, ambapo idadi ya udahili wanafunzi imeongezeka shuleni.

Pia Meneja wa Shule hiyo, Mwita Nchagwa, alisema wao kama wadau wa elimu watamkumbuka sana hayati Rais John Magufuli, katika mchango wake kwenye sekta ya elimu, na kumuomba Rais Samia Suluhu Hassani ayaendeleze yale ambayo ameyaacha hayati Magufuli pamoja na kutetea wanyonge.

Kwa upande wake Kaimu Ofisa elimu Mkoa wa Shinyanga Dedan Rutazika, aliwataka wanafunzi wote hapa nchini wasome kwa bidii na kufikia ndoto zao ili kumuenzi hayati Hayati Rais John Magufuli katika kukuza sekta ya elimu hapa nchini.

TAZAMA PICHA ZA TUKIO HILO HAPA CHINI
Meneja wa Shule ya Msingi na Sekondari Little Treasure, Mwita Nchagwa, akimzungumzia Hayati Rais John Magufuli namna alivyokuza Sekta ya elimu hapa nchini.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasure, Paulo John, akizungumza mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli na mchango wake wa kukuza sekta ya Elimu hapa nchini.
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Little Treasure Comfot Pius, akizungumza mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mwanafunzi Janeth Anthony anayesoma kidato cha tatu katika shule ya Sekondary Little Treasure, akizungumza mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Ofisa elimu mkoa wa Shinyanga Dedan Rutazika, akizungumza mara baada ya wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Little Treasure kumaliza kusaini kitabu cha maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli na kuwaomba wasome kwa bidii ili watimize ndoto zao na kumuenzi Hayati Magufuli kwa vitendo katika kukuza sekta ya Elimu hapa nchini.
Meneja wa shule ya Msingi na Sekondari Little Treasure Mwita Nchagwa, akisaini kitabu cha maombolezo kifo cha Rais John Magufuli katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa shule ya Sekondari Little Treasure Johannes Mwita, akisaini kitabu cha maombolezo kifo cha Rais John Magufuli katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mwalimu wa Shule ya Little Treasure Unice Herman akisaini kitabu cha maombolezo kifo cha Rais John Magufuli katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mwanafunzi Comfort Pius anayesoma darasa la sita katika shule ya Msingi Little Treasure mkoani Shinyanga, akisaini kitabu cha Maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mwanafunzi Janety Athony anayesoma kidato cha tatu katika shule ya Sekondar Little Treasure mkoani Shinyanga, akisaini kitabu cha Maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mwanafunzi Vedastus John, akisaini kitabu cha maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli, katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Little Treasure wakiwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Little Treasure wakiwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli.
Wanafunzi na walimu wa shule ya msingi na Sekondari Little Treasure wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Shinyanga (wa kwanza kushoto) mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha maombolezo kifo cha Hayati Rais John Magufuli, katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga leo.


Post a Comment

0 Comments