Header Ads Widget

MUIGIZAJI MONALISA ATANGAZWA KUWA MSEMAJI WA SIMBA QUEENS

Mlezi wa Simba Queens, Fatema Dewji (kulia) akimtambulisha na kumkabidhi jezi ya klabu hiyo muigizaji Monalisa ambaye sasa atakuwa msemaji wa timu ya wanawake ya Simba, Simba Queens

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, Simba Queens, wamemtangaza rasmi Msanii wa filamu Bongo, Monalisa kuwa Msemaji wa timu hiyo.

Kupitia kwa Mlezi wa Simba Queens, Fatema Dewji amemtambulisha mwanadada huyo nguli katika tasnia ya Filamu nchini na mwenye mafanikio makubwa kwenye upande huo kuwa Msemaji wa timu hiyo.

"Mlezi wetu Fatema Dewji amemkaribisha rasmi Monalisa kama msemaji wa simba queens tunaimani Monalisa atafanya kazi nzuri katika kueneza taarifa zote zinazohusiana na Simba Queens kwenye jamii yetu. Kwa uzoefu wa Monalisa tunaimani atakwenda kuwa msemaji bora wa timu yetu na uzoefu wake aliokua nao katika jamii. Karibu Simba Queens Msemaji Wetu,”  imesema taarifa kutoka Simba Queens.

Simba Queens ina shika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya wanawake Tanzania Bara wakiwa na alama 36 baada ya kushuka dimbani mara 14 wakiwa wametoa sare tatu bila kufungwa.

Ambapo, katika mwendelezo wa ligi hiyo, mabingwa hao watetezi watashuka dimbani Ijumaa Machi 5, mwaka huu kuwavaa watani wao wa jadi Yanga Princess ambao ni vinara wa ligi hiyo kwa sasa.


Post a Comment

0 Comments