Header Ads Widget

MUIGIZAJI LULU AFUNGA NDOA NA CEO WA TVE/EFMNi 'Headlines' za staa wa filamu hapa nchini Tanzania Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye rasmi kabisa siku ya leo Februari 16,2021 amefunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi Francis Ciza 'Majizzo' ambaye ni CEO wa EFM na TVE.

Kupitia picha ambazo zimepostiwa mitandaoni zimeonesha wawili hao wakila kiapo cha kufunga ndoa hiyo ambayo imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Gasper, Mbezi Beach Jijini Dar es Saalm.

Mahusiano ya Elizabeth Michael Lulu na Majizzo ni ya muda mrefu na walikuwa wote kwenye kipindi ambacho Lulu alikuwa na kesi ya kuua bila kukusudia na kufikia Septemba 30, 2018 Majizzo alimvalisha pete ya uchumba Lulu.
Picha na Global Tv

Picha na Global TV

Post a Comment

0 Comments