Header Ads Widget

JAMII YATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUONGEZA THAMANI, KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA

 

Stanley Isaac Manyonyi 

Na Josephine Charles - Shinyanga
Jamii imesisitizwa kutumia mitandao kwa ajili ya kupata maarifa kujenga tabia ya kuongeza thamani, ufanisi na kupunguza gharama za maisha ya kila siku.

Rai hiyo imetolewa na Mtaalamu wa Kompyuta na Teknolojia ya Habari na mawasiliano TEHAMA kutoka Chuo cha Cha Nelson Mandela Kilichopo jijini Arusha Stanley Isaac Manyonyi wakati akizungumza katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja Fm kila Jumatatu hadi Ijumaa saa tatu asubuhi mpaka saa saba kamili mchana. 

Hiyo inatokana na baadhi ya watu kutumia miandao vibaya kwa kuchapisha (kuposti) picha za utupu, kuchapisha picha zenye kuleta madhara kwa kizazi cha baadaye, mfano mama anachati mtoto amelala na mbwa pembeni,wengine kuunguza vyakula wakati wa kupika na kwa akina baba kutokuwajali wake zao kipindi cha ujauzito wanatumia muda mwingi mtandaoni badala ya kuwafariji wake zao. 

Amesema kwa mujibu wa Tovuti ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Takwimu inaonesha kuna ukuaji wa matumizi ya mtandao(internet) hasa kwenye simu ambapo 2013 kulikuwa na watumiaji wa internet milioni 9,2016 wakaongezeka na kufikia million 19 na 2020 mwezi Septemba ongezeko la watumiaji Tanzania likafikia milioni 27.9. 

Amefafanua kuwa kwenye sekta ya TEHAMA kuna ukuaji mkubwa wa matumizi ya Internet ambao unahusisha watu, miundombinu na sera ambazo serikali ya Tanzania inazidi kuweka.

Post a Comment

0 Comments