Header Ads Widget

PICHA: MATUKIO MBALIMBALI SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kutimiza miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar alipowasili katika Viwanja vya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar leo Januari 12,2021 kwa ajili ya kushiriki kwenye Maadhimisho hayo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kwenye Maadhimisho ya miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika leo Januari 12,2021 katika Viwanja vya Mnazi mmoja Mjini zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Aman Abeid Karume kwenye maadhimisho ya miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika leo Januari 12,2021 katika Viwanja vya Mnazi mmoja Mjini zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia suluhu Hassan, leo Januari 12,2021 ameshiriki kwenye Maadhimisho ya miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja Mjini zanzibar.

Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Wananchi na Wanachama wa Vyama mbalimbali vya Siasa wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya muaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12,2021 katika Viwanja vya Mnazi mmoja Mjini zanzibar.

Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Wananchi na Wanachama wa Vyama mbalimbali vya Siasa wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya muaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12,2021 katika Viwanja vya Mnazi mmoja Mjini zanzibar.




Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais

Post a Comment

0 Comments