Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Waziri Mkuu wa Tanzania Dk. Mwigulu Nchemba amefanya ziara katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kata ya Iselamagazi, kwa kuzungumza na wananchi pamoja na kusikiliza kero zao na kuzitatua.
Ziara hiyo imefanyika leo Novemba 9,2026.
Waziri Mkuu akizungumza na wananchi wa Iselamagazi ametoa maelekezo mbalimbali ikiwamo kupiga marufuku wagonjwa kutozwa pesa za kuchangia mafuta ya gari la wagonjwa ambulansi, wajawazito kuwekwa mapokezi kwa muda mrefu wakiambiwa wapeleka beseni pamoja na ndoo.
Maelekezo mengine ni kuruhusu wanunuzi wengi wa zao la pamba, pamoja na kufanyika kwa usanifu upya wa barabara ya kutoka Oldshinyanga hadi Iselamagazi makao makuu ya halmashauri hiyo.
Kesho Waziri Mkuu atakuwa Katika Jimbo la Itwangi kwa Mbunge Azza Hillal Hamad na baada ya hapo ataelekea wilayani Kahama.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA👇👇
Waziri Mkuu Dk .Mwigulu Nchemba akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita alipowasilia katika viwanja ya Iselamagazi wilayani Shinyanga kuzungumza na wananchi.
Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba akisalimia na Mbunge wa Solwa Ahmed Salum.
Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Iselamagazi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum akizungumza.
Mbunge wa Vitimaalumu mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464