` VIJANA WA SENET SHINYANGA WAMETAKIWA KUJITOKEZA KUISEMEA SERIKALI

WANDAMAN HOTEL

VIJANA WA SENET SHINYANGA WAMETAKIWA KUJITOKEZA KUISEMEA SERIKALI

 

 

VIJANA WA SENET SHINYANGA WAMETAKIWA KUJITOKEZA KUISEMEA SERIKALI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Wanachama wa Senet ya vyuo na vyuo vikuu kupitia umoja wa vijana (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga, wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuisemea serikali yao ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo inaongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kutangaza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imetekelezwa pamoja na utoaji wa mikopo kwa wanavyuo.
Rai hiyo imetolewa leo Novemba 29, 2026 na Katibu wa Senet Mkoa wa Mwanza Maua Sabasaba Sarungi, ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana Taifa, wakati akizungumza na wana Senet wa Mkoa wa Shinyanga kutoka Chuo cha Hill Forest, Shycom, St Joseph, Chuo cha Madini na Serikali za Mitaa.

Amesema, vijana wa Senet wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuisemea serikali yao, kwamba wapinzani kila siku wamekuwa wakiikosoa serikali, lakini masuala ambayo wamekuwa wakikosoa yameshatekelezwa lakini vijana hawayasemi, hivyo wanapaswa kuyasema mambo mazuri ambayo serikali imeyafanya na siyo kukaa kimya, na kumwachia Mwenyekiti wa UVCCM Taifa peke yake Mohamed Kawaida.
“Vijana wa Senet mnapaswa kutoka kuisemea serikali na kuzungumza kwa data sahihi, mfano tokea Rais Samia ameingia madarakani upande wa mikopo elimu ya juu, tulikuwa na takribani zaidi ya bilioni 400, lakini mpaka tunapozungumza muda huu bajeti ya mikopo imeongezeka hadi kufika zaidi ya Trilioni Moja, sawa na ongezeko la asilimia 128,” amesema Maua.

Aidha, amewataka pia viongozi wa Senet katika Matawi ya vyuo hivyo, waendelee kukijenga Chama, kujenga mahusiano mazuri na viongozi wa serikali ya wanafunzi, pamoja na kusikiliza changamoto za wanafunzi na kuzitatua.
Katika hatua nyingine, amewataka vijana wawe wanatumia fursa kwenye matukio mbalimbali, ikiwamo kuonyesha vipaji vyao na kuacha kujificha bali wajitokezea, na kwamba uthubutu wao ndiyo kutoka kwao kimaisha na uoga wao ndiyo angamiza lao.

Naye Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Jackson Mwizarubi, amesema dhamira ya umoja huo ni kuwafikia wanachama wao wote vyuoni, pamoja na kutatua changamoto zao ili waweze kufikia malengo yao, na kwamba hakuna mwanafunzi ambaye ataacha chuo sababu ya kupatwa na changamoto yoyote lile, bali wataitatua na mwanafunzi kutimiza ndoto zake.
Aidha, ametangaza kwamba kwa vijana wote wa vyuo na vyuo vikuu, kuwa kuna challenge ambayo imeanzishwa ya kuzungumzia miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa na serikali kwa kijirecord video, na kisha kushare na viongozi wa Senet, na wao kuipelekea ngazi ya juu kwenda kushindanishwa na nyingine ili mshindi apatikane na kupewa zawadi.

TAZAMA PICHA👇👇

Katibu wa Senet Mkoa wa Mwanza Maua Sabasaba Sarungi, ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana Taifa akizungumza.
Katibu wa Senet Mkoa wa Mwanza Maua Sabasaba Sarungi, ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana Taifa akizungumza.
Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Jackson Mwizarubi akizungumza.
Mwenyekiti wa Senet Mkoa wa Shinyanga Jackson Mwizarubi akizungumza.
Katibu wa SENETI Mkoa wa Shinyanga Lukomanga Jinyange akizungumza.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464