Header Ads Widget

JESHI LA POLISI, TVMC NA WADAU WAZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA, DC MBONEKO ATOA WITO KWA WAZAZI


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Debora Magiligimba akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Na Marco Maduhu -Shinyanga
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, kwa kushirikiana na wadau wa watoto likiwamo Shirika la The voice of Margnalize Community (TVMC), linalojihusiha na utetezi wa haki za watoto mkoani hapa, wamezindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Uzinduzi huo umefanyika leo, kwenye viwanja vya Jeshi la Zimamoto Manispaa ya Shinyanga, na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa kupinga matukio ya ukatili ndani ya jamii, likiwamo Shirika la Save the Children, Thubutu Afrika, Agape, Women Fund Tanzania, Pacesh, ICS, na shirika hilo la TVMC.

Mkurugenzi wa Shirika la TVMC, Mussa Ngangala, akizungumza wakati akitoa salam kwenye uzinduzi huo, amesema katika kupambana na matukio ya ukatili dhidi ya watoto zikiwamo mimba na ndoa za utotoni, shirika hilo limepanga kujenga nyumba salama ili kutunza wahanga wa matukio hayo na kutoharibu ushahidi.

Amesema moja ya changamoto ambayo imekuwa ikiwakabili katika kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya watoto hasa mimba na ndoa za utotoni, ni kuharibika kwa ushahidi, na kusababisha watuhumiwa kutofungwa jela, na kuendelea kuwapo kwa matukio hayo.

“Shirika letu la TVMC, tunampango wa kujenga nyumba salama kwa ajili ya kuhifadhi wahanga wa mimba na ndoa za utotoni, ili kutoharibu ushahidi dhidi ya watuhumiwa, na kuwafunga jela ili kumaliza kabisa matukio haya, sababu kesi nyingi zimekuwa zikiishia njiani sababu ya ushahidi kuharibika,”amesema Ngangala.

“Pia tunaiomba Serikali iifanyie marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ili kutokinzana na sheria nyingine ambazo zina mlinda mtoto, sababu sheria hiyo ni mwiba katika kupambana na matukio ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni, ambapo inaruhusu mtoto kuolewa kwa ridhaa ya wazazi au mahakama,” ameongeza.

Naye Mgeni rasmi akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, ameitaka jamii kuachana na matukio ya ukatili dhidi ya watoto, likiwamo suala la ubaguzi la kuwapatia elimu watoto wa kike pamoja na kuwaozesha ndoa za utotoni.

Pia amewataka wazazi kuvunja ukimya na kuzungumza na watoto wao juu ya madhara ya kufanya mapenzi katika umri mdogo, pamoja na kufuatilia mienendo yao muda wa kurudi nyumbani.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Debora Magiligimba, ameitaka jamii kuwa makini na wageni wa kiume, na kutoruhusu kulala chumba kimoja na watoto, na kubainisha kuwa matukio mengi ya ubakaji yamekuwa yakifanywa na watu wa karibu na familia.

Aidha ametaja takwimu za matukio ya ukatili dhidi ya watoto mkoani Shinyanga kwa kipindi cha kuanzia June hadi Agost mwaka huu, kuwa yametokea matukio 231, ambapo kwa mwaka jana yametokea 151 sawa na ongezeko la matukio 80.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia inasema, “TUPINGE UKATILI WA KIJINSIA, MABADILIKO YANAANZA NA MIMI”, ambayo yalianza Novemba 25 na kilele chake ni Decemba 10 mwaka huu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho hayo siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, na kuitaka jamii iachane na matukio hayo ya ukatili.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho hayo siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika kwenye viwanja vya zimamoto mjini Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Debora Magilingimba akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga. Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Ngangala akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Mkurugenzi wa shirika la TVMC Mussa Ngangala, akielezea mipango ya Shirika hilo namna ya kupambana na kutokomeza matukio ya ukatili hasa tatizo la mimba na ndoa za utotoni, kwa kuanzisha nyumba salama ya kuhifadhi wahanga wa matukio hayo, ili kutoharibu ushahidi. Mwakilishi kutoka Shirika la (WFT) Glory Mbia, akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
Mkuu wa upelelezi mkoani Shinyanga (RCO) Davis Msangi akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Shinyanga, Afrikanus Sule,akielezea matukio ya ukatili ambayo yamekuwa yakifanyia kwenye vyombo vya usafiri.

Mkuu wa idara dawati la jinsia la Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Victoria Maro, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili ukiendelea.

Uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili ukiendelea.

Uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili ukiendelea.

Awali maandamano yakiwasili kwenye eneo la uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga matukio ya ukatili.

Maandamano yakiendelea.

Maandamano yakiendelea.

Maandamano yakiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kushoto, akitoa zawadi ya boksi la madaftari na kalamu kwa ajili ya kuwapatia wanafunzi, kulia ni Mwalimu wa shule ya msingi Town Boniphace Malima.
Zoezi la ugawaji madaftari kwa shule ya msingi Mwenge likiendelea.

Burudani ikitolewa kwenye uzinduzi wa maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.


Burudani zikiendelea kutolewa kwenye uzinduzi wa maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko katikati, akipiga picha ya pamoja na wadau wa maendeleo na Jeshi la Polisi mara baada ya kumaliza kuzindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko katikati, akipiga picha ya pamoja na wanafunzi pamoja na walimu mara baada ya kumaliza kuzindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia.









Post a Comment

0 Comments