Header Ads Widget

WANA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA MSALALA WATINGA KISHAPU KUJINOA UANDAAJI BAJETI KWA MRENGO WA JINSIA


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson akizungumza wakati wa ziara ya Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwenye halmashauri ya Kishapu kwa ajili ya kujifunza uandaaji wa bajeti ya mrengo wa kijinsia na umuhimu wake kupitia mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na TGNP. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala kata za Shilela na Lunguya wametembelea halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa ajili ya kujifunza kuhusu uandaaji wa bajeti ya mrengo wa kijinsia na umuhimu wake kupitia mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia shirika la Watu na Makazi Duniani (UNFPA). 

Ziara hiyo ya siku tatu itakayohusisha kutembelea vituo vya taarifa na maarifa katika halmashauri ya Kishapu imeanza leo Jumatatu Desemba 28,2020 kwa Wanavituo vya taarifa na maarifa kutoka wilaya za Msalala na Kishapu kukutana katika kikao kilichofunguliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson. 

Afisa Programu kutoka TGNP, Anna Sangai alisema lengo la ziara hiyo ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia na umuhimu wake,kubadilishana uzoefu na mbinu kuwezesha ushawishi uingizwaji wa masuala ya jinsia katika bajeti na ujenzi wa vuguvugu la pamoja kupitia jamii. 

“Kupitia Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi pia katika ziara hii tutapitia maeneo ambayo viongozi na jamii wamefanikiwa kushawishi uingizwaji wa bajeti ya kijinsia”,aliongeza. 

Alisema Bajeti ya mtazamo wa kijinsia ni bajeti itakayotatua changamoto za makundi yote katika jamii ,inayotoa haki kwa wote na kwamba ni lazima makundi yote katika jamii yafaidi keki ya taifa. 

Akifungua kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson aliishukuru TGNP kwa kazi inayoendelea kuifanya katika jamii kwa kuhamasisha masuala ya usawa wa kijinsia huku akibainisha kuwa Halmashauri yake inatenga bajeti kwa mrengo wa kijinsia. 

Alisema matunda ya TGNP na vituo vya taarifa na maarifa yanaonekana ambapo masuala ya kijinsia yanapewa kipaumbele katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu ili kufikia usawa wa kijinsia kwa asilimia 50 kwa 50. 

“Lakini wanaume wasibaki nyuma katika kufikia usawa wa 50 kwa 50. Tunapozungumzia suala la jinsia tunazungumzia jinsi zote mbili,baba na mama. Kama tukimsema sana mama tukamuacha baba huenda jitihada zisifanikiwe. Jamii pia jamii inatakiwa kuzingatia masuala ya usawa wa kijinsia na kwamba sasa hakuna jambo la mwanamke tu au la mwanamke tu”,alisema. 

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Kishapu, Joseph Swalala alisema licha ya halmashauri hiyo kuzingatia masuala ya usawa wa kijinsia pia alibainisha kuwa bado changamoto ya mimba za utotoni ipo na ili kukabiliana na changamoto hiyo wameanzisha shule maalumu kwa ajili ya wasichana. 

Naye Diwani wa Kata ya Songwa, Abdul Ngolomole alisema mfumo  wa vituo vya taarifa na maarifa vinachangia kuleta maendeleo kwa kasi kubwa katika jamii. 

“Vituo vya taarifa na maarifa vina msaada mkubwa kwani wananchi wanakuwa sehemu ya kuibua vipaumbele na mahitaji yaliyopo katika jamii. Ushirikishwaji wa wananchi umekuwa mkubwa katika masuala ya maendeleo”,alieleza Ngolomole. 

Hata hivyo Mwenyekiti wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilayani Kishapu, Rachel Madundo aliwashauri wana vituo vya taarifa na maarifa kufanya kazi kwa kujituma na kuhakikisha wanashirikiana na kutunza siri hali itayowafanya kuaminika katika jamii. 

Madundo alitumia fursa hiyo kuiomba TGNP kuongeza vituo vya taarifa na maarifa wilayani Kishapu kutokana na wilaya hiyo kuwa na mahitaji mengi.

Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Lunguya, Benedicto Mussa na Mwenyekiti kituo cha taarifa na maarifa kata ya Lunguya katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Loyce Kabanza aliishukuru TGNP kwa kuandaa ziara hiyo akieleza kuwa itawasaidia kuwajengea uelewa na ujasiri zaidi utakaowasaidia kufanya kazi yao vizuri.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson akizungumza wakati wa ziara ya Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwenye halmashauri ya Kishapu kwa ajili ya kujifunza uandaaji wa bajeti ya mrengo wa kijinsia na umuhimu wake kupitia mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na TGNP.Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Kishapu, Joseph Swalala akizungumza wakati wa ziara ya Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwenye halmashauri ya Kishapu kwa ajili ya kujifunza uandaaji wa bajeti ya mrengo wa kijinsia na umuhimu wake kupitia mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na TGNP.
Afisa Programu kutoka TGNP, Anna Sangai akizungumza wakati wa ziara ya Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwenye halmashauri ya Kishapu kwa ajili ya kujifunza uandaaji wa bajeti ya mrengo wa kijinsia na umuhimu wake kupitia mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na TGNP.
Afisa Programu kutoka TGNP, Anna Sangai akizungumza wakati wa ziara ya Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwenye halmashauri ya Kishapu kwa ajili ya kujifunza uandaaji wa bajeti ya mrengo wa kijinsia na umuhimu wake kupitia mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na TGNP.
Afisa Programu kutoka TGNP, Anna Sangai akizungumza wakati wa ziara ya Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwenye halmashauri ya Kishapu
Diwani wa Kata ya Songwa wilayani Kishapu Abdul Ngolomole akizungumza wakati wa ziara ya Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwenye halmashauri ya Kishapu 
Diwani wa Kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Benedicto Mussa akizungumza wakati wa ziara ya Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwenye halmashauri ya Kishapu.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Noela Levira akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Mwenyekiti kituo cha taarifa na maarifa kata ya Lunguya katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Loyce Kabanza akiishukuru TGNP kwa kuandaa ziara hiyo.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Conchesta Kabete akizungumza wakati wa ziara hiyo wilayani Kishapu.
Katibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilaya ya Kishapu, Peter Nestory akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Fredina Said akizungumza kwenye kikao hicho.
Diwani wa kata ya Ukenyenge Underson Mandia ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu akielezea umuhimu wa vituo vya taarifa na maarifa.
Mwenyekiti wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilayani Kishapu, Rachel Madundo akiwasihi wana vituo vya taarifa kushirikiana na kutunza siri wanapotekeleza majukumu yao.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Kikao kinaendelea
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.

Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Msalala na Kishapu wakiwa ukumbini.
Wana Vituo vya Taarifa na Maarifa wa Kishapu wakiwa ukumbini.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments