Header Ads Widget

WATOTO 22 KATA YA MONDO-KISHAPU WABAINIKA KUWA NA UTAPIAMLO


MAGANGA Mfawidhi wa Zahanati Dkt,Christian Ngowi akitoa elimu ya namna ya uandaaji wa chakula chenye lishe kwa akinamama 22 wenye watoto wa utapiamolo katika kijiji cha Wishiteleja Kata ya Mondo, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Na Shaban Njia-Kishapu
UKOSEFU wa elimu ya uandaaji wa chakula chenye lishe katika Kijiji cha Wishiteleja Kata ya Mondo Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga, imesababisha kuwepo kwa watoto wengi wenye ugonjwa wa utapiamlo na upungufu wa wingi wa damu kwa wanawake wajawazito.

Pia Mila na desturi potofu kwa baadhi ya jamii zimekuwa zikimkandamiza mwanamke mjamzito kutumia vyakula vyenye lishe hasa vya jamii ya wanyama kwa ajili ya ukuaji wa mtoto tumboni na kusababisha ukuaji wa mtoto kuwa duni baada ya kujifungua.

Kauli hiyo ilibainishwa jana na Mratibu wa shughuli za lishe Mkoani Shinyanga, Denis Madeleke wakati wa ufuatiliaji wa mradi wa uboreshaji huduma za lishe katika kuimarisha afya ya mama na mtoto (ENRICH) unaotekelezwa Halmashauri tano za Mikoa ya Shinyanga na Singida chini ya World Vision Tanzania kwa ufadhiri wa serikali ya Canada.

Alisema kuwa kijiji cha Wishiteleja kinawatoto 190 wenye umri kuanzia miezi sita hadi miaka miwili, kati ya hao 71 walifanyiwa tathmini na kubaini watoto 22 wenye ugonjwa wa utapiamlo kwa kukosa lishe bora licha ya kuwa na vyakula vya kutoka kwenye maeneo yao.

Aidha Madeleke alisema kuwa ukuaji wa mtoto unaanza wakati mimba inapotunga hadi siku 1000,anapokuwa na udumavu au utapiamlo na kushindwa kumsaidia ndani ya siku hizo,haweza kupona na baadala yake atakuwa na udumavu milele na ndio sababu ya world Vision kutekeleza mradi huo.

Pia alisema kuwa kabla ya utekelezaji wa mradi huo hali ya utapiamlo Mkoa wa shinyanga ulikuwa asilimia 59 kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 na sasa umepungua hadi asilimia 30.4 kwa mwaka 2018,udumavu asilimia 30.2 na ukondefu asilimia 4.

Nae Mratibu wa mradi wa ENRICH, Dkt. Frank Mtimbwa alisema kuwa,mradi huo umeanza kutekelezwa tangu mwaka 2016 katika Halmashauri tano za Mikoa ya Shinyanga na Singida na unatarajia kukamilika machi 2021 na umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 6 dola za Canada.

Alisema kuwa lengo la utekelezaji wa madi huo ni kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wadogo chini ya miaka mitano,nakwamba upungufu wa damu kwa akinamama wajawazito unatokana na upungufu wa lishe wakati wa kipindi chote cha ujauzito.

Kwa upande wake Ofisa Kilimo wa Kata ya Mondo, Pius Maganga alisema,wameanzisha bustani za mbogamboga kwenye kaya 22 zilizobainika kuwa na ugonjwa wa utapiamlo lengo likiwa nikupambana na ugonjwa huo ambao umejitokeza kwa kula vyakula visivyokuwa na lishe.

Mmoja wa wanawake waliobainika kuwa na mtoto wenye utapiamlo, Magdalena John alisema,mtoto wake alikuwa chini ya kg saba na baada ya kupewa elimu ya namna ya kuandaa chakula chenye lishe na kulima bustani za mbogambona Kg za mtoto zinaongezeka kila mwezi na sasa anakg 10. 
 
http://

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mondo iliyopo kijiji cha Wishiteleja Kata ya Mondo,Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, Dkt. Christian Ngowi akimpima uzito mtoto mdogo mwenye umri chini ya miaka mitano kati ya watoto 22 waliobainika kuwa na utapiamolo wilayani Kishapu.


Post a Comment

0 Comments