Header Ads Widget

SAVE THE CHILDREN LAWANOA WADAU SHINYANGA UANDAAJI BAJETI NZURI NGAZI YA HALMASHAURI


Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, akielezea madhumuni ya mradi na mafunzo.

Na Marco Maduhu -Shinyanga
Shirika la Save The Children ambalo linatetea haki za watoto, limetoa mafunzo ya mchakato wa bajeti ngazi ya halmashauri, ili kuisaidia Serikali uaandaaji wa bajeti nzuri ambayo itatoa dira ya maendeleo kwa kuzingatia vipaumbele vya wananchi.

Mafunzo hayo ambayo yatachukua siku mbili kuanzia leo, yameshirikisha watendaji wa Kata, wataalamu kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, waandishi wa habari, pamoja na wadau kutoka mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali,

Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha, Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau mbalimbali katika kushiriki kikamilifu kuandaa masuala ya bajeti, na kutambua wajibu wao katika kushiriki uundaji wa bajeti.

Amesema mradi huo wa masuala ya kibajeti utadumu ndani ya miaka miwili, ambapo ulianza june (2020) na utakoma Decemba (2021), ambao unatekelezwa Zanzibar maeneo ya unguja mjini, magharabi “A” na “B”, Mbozi mkoani Songwe, pamoja na manispaa ya Shinyanga, kwa ufadhili wa Ubalozi wa ulaya.

“Lengo pia la mafunzo haya ni kujenga uwezo kwa watendaji wa Serikali ngazi ya halmashauri, na wadau mbalimbali katika kupata elimu ya mchakato wa kibajeti ya Serikali, na kutambua miongozo inayo simamia michakato hiyo, ili kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa haki za watoto hasa katika masuala ya kiafya, elimu, pamoja na kupinga matukio ya ukatili,” amesema Enock.
 
Naye Mgeni Rasmi akifungua mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoa wa Shinyanga, Joachim Otaru, amewataka washiriki hao wayashike vizuri mafunzo hayo, na kwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo katika uaandaji wa bajeti, kwa kuzingatia vipaumbele vya wananchi pamoja na kushirikisha makundi yote.

“Mafunzo haya ya bajeti ni muhimu sana, sababu yanagusa maisha yetu, hivyo na waomba katika uaandaji wa bajeti ijayo ya Serikali, mshirikishe wadau na makundi yote kuanzia ngazi ya chini,”amesema Otaru.

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo ya kibajeti mchumi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Allex Mpasa, amesema kuwa sasa hivi bajeti hua zinaandaliwa kwa kuzingatia jitihada za wananchi, na siyo kuzingatia vipaumbele vyao, jambo ambalo siyo sahihi.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo hasa watendaji wa Serikali, walishukuru kupewa elimu hiyo ambayo itakuwa msaada mkubwa kwao, katika uaandaji wa bajeti kwa kuzingatia vipaumbele vya wananchi, na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Katibu tawala msaidizi mipango na uratibu mkoani Shinyanga Joachim Otaru,akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, akielezea madhumuni ya mradi na mafunzo.

Mchumi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Allex Mpasa, akitoa elimu ya uaandaaji wa bajeti.


Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
 
 Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoinem akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Afisa mipango mwandamizi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Zanzibar Masika Baraka, akichangia kwenye mafunzo hayo.
 
Grory Mbia ambaye ni mwakilishi wa (UN WOMEN) Mkoani Shinyanga, akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

John Shija kutoka shirika la Paceshi mkoani Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Salum Sudi ambaye ni mtendaji wa Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Victor Kajuna mtendaji wa Kata ya Ibinzamata manispaa ya Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Ponsian Isaack mtendaji wa Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Sara Wamkuru mtendaji wa Kata ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye kazi ya vikundi.

Waandishi wa habari, Malaki Philipo, Suzy Butondo na Greyson Kakuru wakishiriki kwenye kazi ya vikundi wakati wa mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye kazi ya vikundi.

Washiriki wakiwa kwenye kazi ya vikundi.

Washiriki wakiwa kwenye kazi ya vikundi.


Post a Comment

0 Comments