Header Ads Widget

KIWANDA CHA 'SHUJAA' SHINYANGA CHAANZA KAZI BAADA YA MWAKA MMOJA, WAFANYAKAZI 400 WAREJEA KAZINI

Muonekano wa nje wa Kiwanda cha Canon kinachozalisha vinywaji vikali vya SHUJAA, kilichopo mjini Shinyanga ambacho kimefunguliwa na kuanza kazi baada ya kusimama kwa miezi 12.

Na Mwandishi wetu, Shinyanga Press Club Blog 
WAFANYAKAZI zaidi ya 400 waliokuwa wamesimamishwa kazi kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kiwanda cha Canon kinachozalisha vinywaji vikali aina ya SHUJAA cha mjini Shinyanga kufungwa ili kupisha uchunguzi wa serikali kuhusu mashaka yaliyokuwepo juu ya uendeshaji wake, wamerejeshwa kazini baada ya kiwanda hicho kufunguliwa tena na kuanza uzalishaji. 

Shinyanga Press Club Blog imefika katika kiwanda hicho na kushuhudia baadhi ya wafanyakazi waliorejea wakianza kutekeleza majukumu yao huku wakieleza hali ya maisha katika familia zao yalivyokuwa magumu. 

Mmoja wa wafanyakazi hao, Mohamed Hamad ameieleza Shinyanga Press Club Blog kuwa waliteseka kutokana na kukosa ajira kwa muda wa mwaka mmoja kutokana na majukumu waliyokuwa nayo ya kulea familia na majukumu mbalimbali, huku akipongeza hatua hiyo ya kurejesha uzalishaji katika kiwanda hicho kwani umeleta faraja kwa wafanyakazi 400 waliokuwa wanakitegemea. 

Naye Mkurugenzi wa kiwanda hicho, George Marwa ameishukuru Serikali kwa kufikia maamuzi hayo na kuruhusu kiwanda kifunguliwe, ambapo amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kuwasikiliza na kuunda tume kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambayo baadae uamuzi ulitolewa kiwanda kianze kazi na uzalishaji umeanza Novemba 5, mwaka huu. 

“Tulikuwa na wafanyakazi zaidi ya 400 na wote walipotez ajira baada ya kiwanda kufungwa, tunategemea kwa sasa watu wetu watarudi tutaendelea na uzalishaji na kazi zitasonga,” amesema Marwa. 

Kwa upande wake Afisa Mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salehe Bwegege ameeleza kuwa kufungwa kwa kiwanda hicho kwa takribani mwaka mmoja kuliathiri mapato ya serikali, na sasa Manispaa hiyo itanufaika kwa kukusanya mapato ambayo yalikuwa yamesimama. 

Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Kuchibanda Kizito ameeleza kuridhishwa na mazingira ya kiwanda hicho, huku akieleza kuwa uongozi wa kiwanda hicho umeidhia kutoa mapipa ya kutunzia taka kwenye maeneo ya umma na vibanda vitatu vya kupumzikia abiria kwenye vituo vya abiria.
Mkurugenzi wa kiwanda hicho, George Marwa akizungumza baada kiwanda hicho kuanza kazi jana Novemba 8, mwaka huu
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiingia kazini kwa mara ya kwanza baada ya kusimama kwa muda wa mwaka mmoja kupisha uchunguzi
Afisa Mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Salehe Bwegege akieleza namna manispaa hiyo itakavyonufaika baada ya kufunguliwa kwa kiwanda hicho

Wafanyakazi mbalimbali wa kiwanda hicho wakieleza furaha yao baada ya kurejea kazini na kusahau machungu ya kutokuwa na ajira kwa mua wa miezi 12.
Meneja mauzo wa kiwanda cha Canon, Laizer akizungumza

Meneja mauzo wa kiwanda hicho, Laizer akionyesha baadhi ya maeneo ya uzalishaji
Wafanyakazi wakiendelea na shughuli kiwandani hapo kwa mara ya kwanza baada ya miezi 12
Shughuli zikiendelea

Uzalishaji ukiendelea
Wafanyakazi wakiendelea na shughuli za uzalishaji

Shughuli za uzalishaji zikiendelea

Uzalishaji ukiendelea kiwandani hapoPost a Comment

0 Comments