Header Ads Widget

WALIMU WATAKAOSIMAMIA MITIHANI DARASA LA SABA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA WIZI WA MITIHANI

Mwenyekiti wa Chama cha walimu(CWT)Manispaa ya Shinyanga Meshack Mashigala.

Na Shinyanga Press Club Blog 
Chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga (CWT)kimewataka walimu watakaosimamia mitihani ya darasa ya saba kufuata maadili na kujiepusha na vitendo vya wizi wa mitihani,ili kuwaonyesha majibu wanafunzi na iwapo wakibainika kufanya hivyo sheria itachukuwa mkondo wake. 

Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa Chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Meshack Mashigala wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,ambapo amesema walimu wanapaswa kuwa waadilifu kwani wao ndiyo wanaonyesha msingi bora kwa wanafunzi wao. 

Mwenyekiti Mashigala amesema walimu wanatakiwa kufuata maelekezo waliyopatiwa kabla ya kwenda kusimamia mitihani,na siyo kufanya kazi hiyo kwa maslahi yao binafsi kwa lengo la kujipatia chochote ili kuiba mitihani na kuwasaidia majibu wanafunzi. 

“Sisi chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga tutasikitika sana tutakaposikia kuna mwalimu kakamatwa kaiba mitihani ya darasa la saba ambayo inatarajiwa kuanza kufanyika kesho Octoba 7 hadi 8,tunaamini walimu wote mmepatiwa semina elekezi kabla ya kwenda kusimamia mitihani”amesema Mwenyekiti wa CWT. 

Akizungumzia maadhimisho ya siku ya mwalimu duniani ambayo hufanyika kila mwaka Octoba 5,Mwenyekiti Mashigala amesema kuwa amesema kuwa wameshindwa kufanya kutokana na kuwa katika maandalizi ya mitihani ya darasa la saba na kwamba wamepanga kwa Mkoa wa Shinyanga kuadhimisha Octoba 16 mwaka huu. 

Mwenyekiti Mashigala amesema katika kuadhimisha siku hiyo wamepanga shughuli mbalimbali kufanyika pamoja na burudani kwa wapenzi wa michezo, ili kuimarisha afya za watumishi wa umma hasa sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kueleza changamoto zinazowakabili walimu katika kutekeleza majukumu yao. 

Post a Comment

0 Comments