Header Ads Widget

MAWAKALA WAKUU NA WASIMAMIZI VITUO VYA KUPIGIA KURA KISHAPU WASISITIZWA KUFUNGUA MAPEMA

Mawakala wakuu na wasimamizi wa uchaguzi wilayani Kishapu wakiekezwa jinsi ya kusimamia wananchi kupiga kura 

Na Suzy Luhende, Shinyanga
Mawakala wakuu na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura wametakiwa kuzingatia muda wa kufungua kituo cha kupigia kura na muda wa kufunga ikiwa ni pamoja na kuhakikisha orodha ya majina iliyobandikwa ifanane majina na yaliyomo kwenye daftari la mpiga kura.

Hayo yamebainishwa jana na Jastine Mpira ambaye ni msimamizi wa kituo kwenye semina ya elekezi ya mawakala wakuu na wasaidizi wa vituo vya kupigia kura katika ukumbi wa Shirecu wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mpira alisema msimamizi wa kituo ndiye mkuu wa kituo cha kupigia kura na atakuwa na jukumu la kusimamia kura na kuhakikisha utulivu na usalama unakuwepo katika kituo cha kupigia kura.

“Wajibu wa msimamizi wa kituo ni kupokea vifaa kwa ajili ya uchaguzi katika kituo husika kuandaa na kufungua kituo cha kupigia kura vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja kamili asubuhi na kufungwa saa kumi jioni,”alisema Mpira.

Aidha alisema msimamizi anatakiwa kutoa ushauri na maelekezo kwa wapiga kura pale inapohitajika na kufunga zoezi mara baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika, pia mawakala waliopo kituoni wanatakiwa kuhakikisha wanapatiwa fomu namba 14 na fomu namba 16 ambayo itawaongoza.

“Msimamizi anatakiwa kushughulikia malalamiko yanayojitokeza kituoni na Kukamilisha fomu zote za malalamiko na kukabidhi kwa msimamizi wa uchaguzi au msimamizi msaidizi”alisema Mpira.

Baadhi ya wasimamizi wa vituo ambao walipatiwa mafunzo Emmanuel Samweli na Juliana Maige walisema mafunzo hayo ya kuelekezwa jinsi ya kusimamia wapiga kura yatawasaidia,hivyo watasimamia vizuri na watalinda amani.

Kwa upande wake msimamizi mkuu wa uchaguzi katika wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson alisema wasimamizi wa vituo wapo 460, wasimamizi wasaidizi wa kwanza 460, na wasimamizi wasaidizi wa pili ni 460 jumla wapo 1380.

“Tumesimamia vizuri wasaidizi na mawakala wa uchaguzi wamepata mafunzo vizuri kwa wakati hivyo tunaamini watasimamia vizuri na uchaguzi katika wilaya yangu utakuwa ni wa amani kabisa hivyo tunawaomba wananchi wenye sifa wajitokeze wote ili waweze kupiga kura”alisema Johnson.
Jastine Mpira akiwafundisha Mawakala wakuu na wasimamizi wauchaguzi wilayani Kishapu jinsi ya kusimamia wananchi kupiga kura tarehe 28
Wakielekezwa jinsi ya kuwasaidia wapiga kura jinsi ya kupiga kura siku ya tarehe 28





Post a Comment

0 Comments