Header Ads Widget

GULAM MUKADAM AFUNGA KAMPENI MJINI, AKIAHIDI KUBADILISHA MAISHA YA WANANCHI KIUCHUMI


Mgombea Udiwani Kata ya Mjini Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya CCM, Gulam Hafeez Mukadam akiomba kura kwa wananchi leo katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni uliofanyika mtaa wa Buzuka.

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mgombea Udiwani Kata ya Mjini Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gulam Hafeez Mukadam, ameahidi wananchi wa Kata hiyo, kuwa endapo wakimchagua kuwa diwani wao siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, atabadili maisha yao na kukua kiuchumi. 

Mukadamu amebainisha hayo leo, wakati akifunga rasmi kampeni zake za kunadi Sera kwa wananchi wa Kata hiyo, mkutano uliofanyika kwenye mtaa wa Buzuka, ambao ulihudhuliwa pia na makada wa CCM. 

Amesema wakati akifanya kampeni za nyumba kwa nyumba kuomba kura, alikumbana na changamoto ya wananchi kutokuwa vizuri kiuchumi, hali iliyomfanya kuguswa nayo, na kuahidi kuwainua kiuchumi wananchi wote wa Kata hiyo ya mjini. 

“Siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, mkanipigie kura nyingi za ushindi, ili niwe diwani wenu kwa awamu nyingine tena, ambapo nimeahidi kuwa inua wananchi wote wa Kata ya mjini kiuchumi, kupitia mikopo ya halmashauri asilimia 10, Nne kwa akinamama, na vijana, na asilimia Mbili kwa walemavu,”amesema Mukadam. 

“Mnacho paswa kwa sasa ni kuunda vikundi, kuandaa katiba yenu pamoja na kufungua akaunti benki, ambapo mimi nitasimamia zoezi zima la kupata mikopo hiyo ambayo haina riba, na mtafanya shughuli mbalimbali pamoja na kufungua viwanda vidogo na hatimaye kuinuka kiuchumi,”ameongeza. 

Pia amesema ataendelea kuwaletea maendeleo wananchi kama alivyofanya kwenye awamu iliyopita, na kuibadilisha Shinyanga kuwa jiji, ambapo Kata hiyo ya mjini ndio kitovu cha mkoa wa Shinyanga. 

Naye Mgombea Udiwani wa Viti Maalum Manispaa ya Shinyanga (CCM) kupitia Kata hiyo ya mjini, Ester Makune, amewataka wananchi siku ya uchaguzi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura, na kuwapigia wagombea wote wa (CCM) ambao ndio watawaletea maendeleo. 
Mgombea udiwani Kata ya mjini manispaa ya Shinyanga (CCM),Gulam Mukadam, (kulia) akiwa na Mgombea udiwani wa vitimaalum Ester Makune wakiapa kuwatumikia wananchi mara baada ya kupata ushindi Oktoba 28.
Aliyekuwa mtia nia wa kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Shinyanga mjini Abdulmaliki Ibrahim, (kulia), akimnadi kwa wananchi Mgombea udiwani Kata ya mjini manispaa ya Shinyanga Gulam Mukadamu, ili wamchague kuwa diwani wao Oktoba 28 mwaka huu siku ya uchaguzi.
Mgombea udiwani wa vitimaalum manispaa ya Shinyanga kupitia Kata ya mjini Ester Makune akiomba kura kwa wananch wa Kata hiyo siku ya uchaguzi wakawapigie kura wagombea wote wa CCM.
Aliyekuwa Mtiania wa kugombea nafasi ua ubunge jimboa la Shinyanga mjini Jimotoli Jilala, akizungumza kwenye mkutano huo wa kufunga Kampeni.
Aliyekuwa Mtia nia wa kugombea nafasi ya udiwani Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo, akizungumza kwenye mkutano huo wa kufunga Kampeni.
Makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kufunga Kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kufunga kampeni.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano wa kufunga Kampeni ukiendelea.

Post a Comment

0 Comments