Header Ads Widget

JPM AZINDUA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI KILIMANJARORAIS John Magufuli, leo Oktoba 22, 2020, amezindua kiwanda cha bidhaa za ngozi kilichopo mkoani Kilimanjaro.

TAARIFA FUPI YA MRADI
Mkurugenzi PSSF: Ujenzi wa mradi huu ni utekelezaji wa maelekezo yako uliyoyatoa tarehe 9 Mei 2016 uliyoyatoa wakati wa ufunguzi wa majenga ya vitega uchumi wa mifuko ya hifadhi ya jamii jijini Arusha, katika hotuba yako ulituelekeza kuwekeza zaidi katika viwanda badala ya kuwekeza tu katika majengo.

Katika kutekeleza, Mei 2017 mfuko kwa kushirikiana na Jeshi la magereza tulianzisha kampuni ya ubia inayojulikana Karanga Leather Industries Company Limited ambayo kwa kwa sasa inajulikana kama Kilimanjaro International Leather Industries yenye mtaji wa bilioni 70 inamilikiwa na mfuko wa PSSF kwa asilimia 86 na Jeshi la Magereza kwa asilimia 14. Jeshi la Magereza likiwa limechangia eneo la kiwanda lenye ekari 25 pamoja na kiwanda cha zamani.

Mfuko wa PSSF unachangia gharama za ujenzi wa majengo, ununuzi wa mashine na mitambo na gharama za uendeshaji. Ujenzi huu unasimamiwa na wataalam wa ndani kupitia taasisi za umma.

Mkandarasi wa ujenzi ni Jeshi la Magereza kwa kiasi cha bilioni 27, mashine na mitambo vimenunuliwa nchini Italy kwa gharama ya Euro milioni 23.6, takribani bilioni 60 zikijumuisha gharama za usafirishaji, ufungaji wa mashine, mafunzo na ushuru wa forodha. Mpaka kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu bilioni 136.

MAGUFULI: Kuanzishwa kwa kiwanda hiki, mimi nina uhakika sasa baada ya mwaka mmoja, miwili tukikutana hata katika kusheherekea, nina uhakika tutakuwa tumevaa viatu vitavyokuwa vimetengenezwa hapa Kilimanjaro.

Wafungwa lazima watumike katika kuzalisha mali, ukifungwa lazima ukatumike vizuri ili ujutie makosa yako ili siku nyingine usifungwe tena na ukishatoka hapa utatoka umeshajua kuzalisha viatu ukafungue kiwanda chako. Kufungwa ni sehemu ya mafunzo.

Nizipongeze pension fund zetu, PSSF na bodi yake pamoja na mkurugenzi mmeanza vizuri sana kwa sababu siku za nyuma pension fund zilikuwa zinawekeza kwenye majengo tu na kule ndiko kulikuwa na percentage nikasema masuala ya kuwekeza kwenye majengo uachwe. Utakuta jengo limejengwa kwa mabilioni, wapangaji wapo nusu tu, faida yake ni ndogo.

Ukiwekeza kwenye viwanda faida yake ni kubwa. Kiwanda hiki kitakuwa kinatoa ajira ya watu elfu tatu. Ungejenga jengo lisingetoa ajira ya watu 3,000 na hawa ni wale watakuwa wanafanya permanently hapa. Wale wengine watakaokuwa wanaleta vyakula, ngozi kwa nchi nzima unaweza ukajikuta umetengeneza ajira ya zaidi ya watu milioni moja.

Mwisho Rais Magufuli amezindua kiwanda na kununua viatu kadhaa vikiwemo vya mke wa askofu, mwandishi wa habari nk. Wakati akinunua viatu hivyo, Magufuli ametania kwa kusema kuwa namba za viatu anavyovaa mkewe, Janeth, ni kubwa na kwamba amezisahau bila hivyo angemnunulia.

Post a Comment

0 Comments