Header Ads Widget

TAWA YAKABIDHI JENGO KWA OFISI YA TAIFA YA MASHITAKA WILAYANI KAHAMA


Kulia ni Kaimu Kamishina wa Wanyamapori nchini Mabula Nyanda  akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini Biswalo Mganga hati ya makabidhiano ya jengo lililokuwa likitumika na Mamlaka ya wanyamapori kanda ya Kigosi na kupewa kwa muda litumike kama  ofisi ya DPP wilaya ya Kahama.

Mamlaka ya Wanyamapori   Tanzania (TAWA) imeikabidhi ofisi ya taifa ya Mashitaka chini ya DPP   jengo lililokuwa likitumiwa na mamlaka hiyo kanda ya Kigosi lililopo wilayani kahama mkoani  Shinyanga, baada ya mapori waliyokuwa wakiyasimamia kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi  za taifa ambapo jengo hilo litatumika kuendesha kesi za jinai ikiwa ni mkakati wa serikali wa kupunguza Msongamano wa  maabusu na waafungwa  katika  Magereza nchini.

Akizugumza Jana baada ya Makabidhiano ya jengo hilo Kaimu Kamishina wa uhifadhi nchini Mabula  Nyanda amesema kuwa kutokana na uhusiano  uliopo kati ya  ofisi yake na ofisi ya DPP  wamekuwa wakishirikiana katika masuala ya uendeshaji wa kesi za makosa  yaliyokuwa yakihusika na rasimali za wanyama pori ambapo   wameamua kuwapatia  jengo  hilo kwa muda ili waweze kusaidia jamii katika kesi mbalimbali

Kama mnavyojua moja ya kazi muhimu sana katika taasisi hizi ni ulinzi wa rasimali za wanyamapori ambazo ni kazi za hima sheria ziko nne kwanza kuna operation, ukusanyaji wa taarifa, uendeshaji wa mashitaka na upelelezi hizi zote zinahusika na mashitaka,”amesema  Kaimu Kamishina Nyanda  

Amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana sana na ofisi ya taifa ya mashitaka katika kesi zote ikiwemo zinazohusu usimamizi wa rasilimali za wanyamapori ambapo DPP amekuwa msaada mkubwa wa kupambana na uharifu kwenye  ujangili,mifugo na uvamizi wa mapori ya akiba hivyo tumeona umuhimu wa kuwapa jengo hili.

Sisi tulikuwa tunatumia ofisi hii ya Kanda ya kigosi toka hapa Kahama baadae serikali ikapandisha hadhi mapori hayo toka pori la akiba hadi  kuwa hifadhi, hivyo tukaaamua kupisha na tulikuwa na mpango wa kuwekeza  mradi, ndipo tukapokea maombi toka kwa mdau wetu muhimu ofisi ya DPP wakitaka tuwapatie kwa ajili ya kufungua ofisi ya taifa ya  mashitaka ya wilaya ya kahama  nasi hatukuwa na shida tukaamua kumpa kwa muda kwa ajili ya utekeleza wa kazi zake za kuhudumia wananchi”

Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini Biswalo Mganga  amesema  kuwa kutokana na idadi kubwa ya  watu walikuwa wakisafiri kwenda kupata huduma mkoani Shinyanga  hali ambayo ilikuwa inachangia kuchelewa kutolewa kwa maamuzi hivyo kusogezwa kwa huduma hiyo wilayani kahama itasaidia kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu.

Tumeamua kufungua ofisi hapa kwa sababu gereza la kahama linapokea watu wengi linapokea kutoka wilaya jirani za Mbogwe na Bukombe zilizoko Mkoani  Geita  hivyo kuna kesi ambazo hazina ulazima sana wakili wa serikali atazichuja na kuzitoleea maamuzi na yale  yanayoshindikana yanakuja kwetu

Biswalo amesema kuwa uwepo wa ofisi hiyo wilayani kahama utasaidia kupunguza  Msongamano  ulioko kwenye gereza hilo pamoja na kuhakikisha kwamba kesi zinaendeshwa mapema na kwa mujibu wa sheria huku ofisi yake ikiendelea na mkakati wa kuwa na majengo yake.

Naibu Katibu Mkuu wizara ya katiba na sheria Amon Mpanju amesema kuwa nchi haiwezi kuwa na amani pasipo uwepo wa ofisi ya Taifa ya mashitaka  hivyo  uwepo wake ni muhimu sana katika kuhakikisha amani inadumu  huku akibainisha kuwa mara baada ya kutembelea gereza la kahama  ni jambo jema lililofanywa na DPP la kuomba kupewa jingo kwa ajili ya kuanzisha ofisi hiyo.

Ni vema ushirikiano huu ukaendelezwa kati  ya TAWA na ofisi ya Mashitaka nchini kuhakikisha  Ulinzi wa Rasilimali za nchi zinaendelea kulindwa na kutunzwa kwa mujibu wa sheria za nchi nimefurahi sana kwa hili lililofanyika leo kuamua kuwapa jengo hili ofisi ya Mashitaka  nanyi hakikisheni mnalitunza ili hata mkiondoka libaki katika ubora  wake

Naye katibu tawala wa wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya  amesema kuwa kwa sasa wilaya hiyo ina idadi  kubwa ya wakazi takribani milioni moja hali inayochangia kuongeza vitendo vya uharifu na ongezeko la makosa ya jinai hivyo uwepo wa Ofisi hiyo   utasiadia kuondoa kero  kwa wananchi ikiwemo ucheleweshwaji wa kesi.

Mkuu wa Magereza Mkoani Shinyanga, Kamishina Msaidizi Elizabeth Mbezi amesema iwapo itaanza kufanya kazi ofisi ya mshitaka ya taifa  wilayani Kahama itasiadia kupunguza kesi za watuhumiwa ambao hawana ulazima sana wa kukaa gerezani pamoja kupunguza Msongamano wa Mahabusu ndani  ya gereza

Kwa sababu  Gereza letu la Kahama linapokea watuhumiwa toka halmashauri tatu wa wilaya hii pamoja na wilaya jirani za Mbogwe na Bukombe ambao hutumia gereza hilo kwa hiyo ifsis hii itasiadia kurahisisha mahabusu ambao si lazima kwenda gerezani kesi zao zikaishia nje”amesema Mbezi.

habari picha 
 Kaimu Kamishina wa Wanyamapori nchini(TAWA) Mabula Nyanda akizngumza mapema kabla ya kukabidhi jengo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini(DPP) Biswalo Mganga akizungumza na viongozi  na watendaji wa Tawa  hawapo pichani.

baadhi ya watendaji wa ofisi ya Mashitaka na ofisi ya  mamlaka ya wanyamapori wasikiliza maelezo ya namna kukabidhiana jengo hilo  
 Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini(DPP) Biswalo Mganga akisaini hati ya makabidhiano ya jengo pamoja na Kaimu Kamishina wa Wanyamapori nchini(TAWA) Mabula Nyanda mbele ya Naibu katibu Mkuu  wizara ya katiba na Sheria Amon Mpanju 
 Naibu katibu Mkuu  wizara ya katiba na Sheria Amon Mpanju akizungumza na viongozi na watendaji wa ofisi  za DPP,Tawa na Ofisi ya upelelezi Mkoa wa Shinyanga na Wilaya ya Kahama

 kamishina Msaidizi Mwandamizi mamlaka ya Wanyamapori nchini (TAWA) akieleza mambo mbalimbali juu ya ushirikiano wao na Ofisi ya (DPP) katika kuendesha Kesi 
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Mashitaka Nchini (DPP) Edson Makallo akizungumza namna ambavyo ofisi yake itaklitunza vizuri jengo hilo ili liweze kutoa hduma zilizokusudiwa na wananchi kupata haki mapema 
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju  walio kaa kwenye wa tatu kutoka Kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali  mara baada ya makabidhiano ya jengo litakalotumiwa na ofisi ya DPP wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga 
jengo la mamlaka ya wanyama pori lililokuwa likitumiwa kama ofisi ya kanda ya kigosi baada ya baadhi ya mapori yaliyokuwa yakisimamiwa kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi za taifa sasa limekabidhiwa kwa mwendesha mashitaka mkuu  wa serikali DPP ili liweze kutumika kutoa huduma kwa wakazi wa Kahama,Mbogwe na Bukombe  ili kupunguza msongamano kwa maabusu katika Gereza la Wilaya ya Kahama.