Header Ads Widget

SAKATA LA KAGERE NA KOCHA WAKE, SIMBA YASEMA NI PROPAGANDA


Kocha wa Simba SC, Sven Vandenbroeck

Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho (ASFC) Simba SC, umekanusha taarifa zilizoandikwa na kuripotiwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii na vyombo vya Habari kuwa mshambuliaji wao Meddie Kagere amepigana na Kocha wake Sven Vandenbroeck.

Taarifa zilizotolewa kwenye mitandao ya kijami na baadhi ya vyombo vya habari, zimeeleza kuwa wawili hao walipigana wakiwa mazoezini, mjini Mbeya baada ya kuwasili wakitokea Arusha kupitia Dar es salaam.

Mkuu wa idara ya habari na mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Manara amesema taarifa hizo sio za kweli, kwani zina lengo la kuvuruga amani ndani ya kikosi chao ambacho kipo tayari kuanza kutetea taji la Tanzania Bara mwishoni mwa juma hili dhidi ya Ihefu FC.

Manara amesema ndani ya kikosi cha Simba kuna amani na furaha kubwa, na hakujawahi kutokea ugomvi wa aina yoyote kama ambavyo taarifa zimeripotiwa.

”Wanasema jana ugomvi uliotokea mazoezini, lakini Simba hawakuwa na mazoezi baada ya mchezo wa ngao ya jamii, hizo ni propaganda ya kuvuruga utulivu uliopo ndani na nje ya Simba, wakitaka itokee kama upande wa pili yanayoendelea”


”Kama idara ya Habari na Mawasiliano hatutokubali kuona watu wanaandika uzushi kuhusu Klabu yetu na tutachukua hatua kali dhidi ya watakaohusika”

Kumekua na taarifa kuwa Kagere ambaye ndiye mfungaji bora wa Ligi kuu kwa misimu miwili mufululizo aligombana na Kocha baada ya kuhoji kwa nini hapewi nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.