Header Ads Widget

TAKUKURU MANYARA YAMNASA MTUMISHI BARAZA LA ARDHI KWA KUOMBA RUSHWA YA SH 100,000

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Manyara inamshikilia Ruth Raniel Semkuyu ambaye ni mtumishi wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Babati kwa makosa ya kudai na kupokea rushwa ya Sh Laki moja (100,000) kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari zilizotolewa Septemba 9, 2020 na Mkuu wa Takukuru Manyara, Holle Makungu ilisema kuwa Ruth alikamatwa baada ya mmoja ya watu walioshinda kesi katika moja ya mabaraza ya Kata mkoani Manyara kufika Takukuru kutaka kukazia hukumu.

Soma zaidi taarifa hiyo hapa chini