Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi imeanza utaratibu
mpaya wa kufanya mikutano jumuishi inayowahusisha viongozi wa mitaa na mashina
nya chama hicho, viongozi wa kata na matawi ya CCM, viongozi na watendaji wa
serikali wanachama wa CCM Pamoja na Wananchi kwa ujumla wao lengo likiwa ni
kuhakikisha chama kinakua na uhai halisi kwa kusikiliza kero za wananchi na
kuzitatua.
Na Mwandishi wetu, Kishapu
Akizungumza katika mkutano huo jumuishi uliofanyika katika
tarafa ya Mondo Wilayani Kishapu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bw.
Mabala Mlolwa amesema dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan kupitia Chama cha
Mapinduzi ni kuhaklikisha kero za wananchi zinatatuliwa sambamba na upatikanaji
wa huduma stahiki kwa wakati
Hata hivyo katika mkutano huo wananchi wa Wilaya ya Kishapu
mkoani Shinyanga wamewasilisha kero zao mbele ya kamati ya Siasa ya CCM ikiongozwa
na mwenyekiti Mabala Mlolwa na kati ya kero hizo ni Pamoja na ukosefu wa
majisafu na salama katika kata ya seke Bugoro, vyeti vya kuzaliwa kukosekana
katyika vituo vya afya na zahanati watoro wanapozaliwa, Changamoto ya
kujiandikisha vitambulishio vya Nida Pamoja na Bima ya Afya na kero ya Mnunuzi
mmoja wa zao la pamba tofauti na zamani kulipokuwa na soko huria linalojumuisha
wanunuzi wengi.
Aidha wananchi hao wamesema kero hizo zimekuwa zikiathiri
shughuli zao za uzalishaji mali, huku Afisa Tawala wa Wilaya ya Kishapu Bw.Fadhili
Mvanga kwa niaba ya Mkuu wa Wilata hiyo Peter Masindi akieleza kuwa serikali
inaendelea kuboresha huduma hizo ili kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi
katika maeneo yao ambapo amefafanua kuwa swala la maji ya ziwa Victoria kufikishwa
katika kata ya Seke tayari limeshafanyiwa Upembuzi yakinifu na utaratibu
unaendelea.
Diwani wa kata ya SekeBugoro Mh. Ferdnand Mpogomi amesema
Changamoto kubwa ya kata hiyo ni ubovu wa Miundombinu ya Barabara lakini pia
swala la mnunuzi mmoja wa zao la Pamba limekuwa likidhoofisha juhudi za
wananchi kulima zao hilo kwakuwa bei ya kilo ya Pamba imekuwa inaporomoka siku
baada ya siku kutokana na wanunuzi wanavyojipangia wenyewe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala
Mlolwa amewataka watendaji wa serikali kuhakikisha wanatoa elimu sahihi kwa
wananchi namna ya upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa kuwasikiliza na
kuhakikisha wanatatua kero wanazoziweza kwa
wakati na kero ambazo hawazi kuzitatua wao ka wao wazifikishe sehemi husika ilinazo
zitatuliwe mara moja.
Aidha Mwenyekitui wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amweataka
viongozi wa Chama ngazi zote kuanzia Mkoa hadi mashina kuchukua utaratibu wa
vikao na mikutano jumuishi kama nyenzo ya utatuzi wa kero na changamoto
zinazoibuliwa na wananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464